Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha
Mbunge
 wa Jimbo, la Kibaha Mjini Silvestry Koka amefanya ziara ya kushtukiza 
kwenye Ujenzi wa Kituo Cha Afya Kongowe ,kitakachogharimu Tsh Mil .400 hadi kukamilika kwake.
Akiwa
 katika eneo la tukio, Koka amezisisitiza kamati za usimamizi wa Ujenzi 
huo kuwa wazalendo na kuheshimu pesa ya serikali huku akihimiza miradi 
kukamilishwa kwa wakati lengwa.
Hata hivyo amewataka wajumbe wa kamati hizo na Viongozi kusimamia Ujenzi sambamba na kuzingatia thamani ya pesa. 
Koka
 alieleza, kituo hicho kinajengwa kwa fedha za mapato ya ndani ya 
Halmashauri ya Mji Kibaha, ambapo kinatarajiwa kukamilika Julai Mwaka 
huu na kuwanufaisha wakazi wa kata ya Kongowe na maeneo jirani.
Pamoja
 na hilo, alialikwa katika Mkutano Mkuu wa CCM kata ya Kongowe kuwa 
Mgeni rasmi na amewapongeza Viongozi wote wanaomaliza muda wao, na 
kuwahamasisha wanachama  wenye nia wagombee kwa uadilifu Ili kuendelea 
kukijenga na kukiimarisha chama .
Vilevile
 amegawa vyeti kwa wanachama na Viongozi mbalimbali wa kata hiyo 
waliofanya kazi za chama vizuri, akiwemo diwani viti maalum Kibaha, 
Lidya Mgaya, vyeti ambavyo vilivyoandaliwa na Kamati ya siasa ya kata 
hiyo ,:;Pia Koka amekabidhi viti 25  vya plastiki vyenye thamani ya Tsh 
450,000/- kwenye mradi wa Vijana wa kata hiyo.



No comments:
Post a Comment