HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, March 28, 2022

KOKA ATOA SIMU JANJA 14 URAHISISHA KUSAJILI KWA NJIA YA KIDIGITAL WANACHAMA WA CCM KIBAHA MJINI

 

Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha
MBUNGE wa Jimbo la Kibaha Mjini Silvestry Koka ,ametoa simu janja 14 kwa ajili ya kusajili kwa njia ya Kidigitali wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ili zirahisishe usajili wa wanachama wa zamani na wapya kisasa.

Akizungumza na viongozi wa sekretarieti za kata kwenye Jimbo hilo Mbunge huyo alisema, wakati chama kinaelekea kuchagua viongozi wake lazima itambue wanachama wake kidigitali.

Alieleza kuwa kila kata itapata simu moja ndiyo sababu ameamua kuunga mkono chama kutambua wanachama wake.

Mgeni rasmi katika kikao hicho ambaye ni katibu wa CCM mkoa wa Pwani ,Said Goha alisema kuwa simu hizo zitasaidia kwenye usajili wa wanachama.

Goa alisema kuwa wilaya hiyo ilikuwa ya mwisho kwenye usajili wa wanachama kwa njia hiyo kati ya Wilaya tisa za mkoa huo.

Alisema kuwa moja ya changamoto walizokuwa nazo ni ukosefu wa simu za kusajilia wanachama.

Naye Diwani wa Viti Maalum Selina Wilson alisema kuwa msaada huo utasaidia kwani walikuwa na wakati mgumu kujichangisha hadi kununua simu hizo.

Wilson alisema kuwa watashirikiana na viongozi wa kata ili kusajili wanachama kwenye maeneo yao.

Kwa upande wake mwenyekiti wa CCM kata ya Kongowe Simon Mbelwa alisema kuwa watapita mtaa kwa mtaa ili kuwafikia wanachama wote.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad