HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, March 28, 2022

Jukwaa la Wajasirimali kuunguruma Mei Dar es Salaam

 

Meneja Mradi wa Jukwaa la Wajasiriamali Fredy Leopold akizungumza kuhusiana na Jukwaa la Wajasiriamali litalofanyika Mei 6 mwaka huu,jijini Dar es Salaam.

Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
WAJASILIAMALI katika Mkoa wa Dar es Salaam wametakiwa kujitokeza katika Jukwaa la Wajasirimalo litalofanyika Mei 6 Mwaka huu katika Ukumbi wa Traveltine Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa Habari Meneja Mradi wa Jukwaa la Wajasiriamalo Fredy Leopold amesema lengo hilo ni kuwakutanisha wajasirimali kwa pamoja na kujua changamoto wanazokutana nazo na kuweza kutatua.

Amesema kuwa katika jukwaa hilo litakwenda sambamba na maonesho ya bidhaa ikiwa ni pamoja kuweza kutafuta masoko ya bidhaa hizo.

Leopold amesema wajasiriamali wanajituma lakini changamoto yao ni masoko hivyo wakiwa katika jukwaa wataun6lganishwa na masoko kwa kutengeza mawasiliano mapya.

Leopold amesema katika amesema jukwaa hilo kutakuwepo na walimu wa kufundisha namna ya kuweza kutengeneza masoko ya kuwa endelevu na sio kuwa na masoko msimu.

"Tunatambua changamoto za wajasiriamali lakini hatuwezi kumfikia kila mmoja hivyo jukwaa ndio chombo cha kukutanisha kila mmoja na hatutamani mtu akose jukwaa hilo kwa mjasirimali wa kutaka kukuza biashara" amesema Leopold.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad