HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, March 27, 2022

DKT. STERGOMENA ATEMBELEA NA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO TANGA

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb) alivyowasili kukagua na Kujionea Ujenzi wa Miundombinu ya Uwanja wa ndege eneo la Shule ya Anga ya Kijeshi (SAK) Jijini Tanga.


 WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mheshimiwa Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb) ametembelea na kukagua miradi ya maendeleo` inayosimamiwa na Wizara ya ulinzi na JKT jijini Tanga.

Miradi aliyoitembelea na kukagua hatua za ujenzi wake ni pamoja na uboreshaji wa uwanja wa ndege wa Jeshi na maabara ya mafunzo.

Kwa upande wa mradi wa uboreshaji wa uwanja wa ndege unajumuisha ujenzi wa karakana ya ndege, mitaro ya maji ya mvua  uzio kuzunguka uwanja huo, nyumba ya Mlango Mkuu wa Kiteule cha Shule ya Anga ya Kijeshi (SAK).

Kipindi cha utekelezaji wa mradi huu ni mieizi sita ambapo ujenzi wake ulianza tangu tarehe 24 Novemba, 2021 na unatarajiwa kukamilika ifikapo tarehe 24 Mei,2022. Mradi utakapokamilika utakuwa umegharimu jumla ya Shilingi 1,829,410,538.56.

Aidha, Dkt. Stergomena alitembelea pia, mradi wa maabara ya mafunzo katika Shule ya Kijeshi ya Ulinzi wa Anga (SKUA) iliyopo jijini Tanga.

Miradi yote miwili inatekelezwa na Kampuni ya Ujenzi ya SUMAJKT (SUMAJKT Construction Company Limited) Kanda ya Kaskazini akiwa ni mkandarasi, Mshitiri ni Wizara ya Ulinzi na JKT na Mshauri Mwelezi ni MOD Consulting Unit, Kitengo chini ya Wizara.

Waziri Tax akipewa ripoti ya Mwendelezo wa Mradi wa Ujenzi wa Miundombinu ya Uwanja wa Shule ya Anga ya Kijeshi (SAK) Jijini Tanga, Mhadhara huo ukiyolewa na Mwakilishi wa Mkandarasi kutoka SUMAJKT.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt Stergomena Lawrence Tax (Mb) akikagua Gwaride la Mapokezi mara baada ya Kuwasili Shule ya Kijeshi Ulinzi wa Anga (SKUA) Jijini Tanga
Mwonekano wa nje wa Jengo jipya lililojengwa kwa ajili ya  Maabara ya Shule ya Kijeshi ya Ulinzi wa Anga (SKUA) Jijini Tanga.

Pichani ni Marubani na Wakufunzi wa Shule ya Anga ya Kijeshi (SAK) Wakitoka Uwanjani mara baada ya kufanya onyesho mbele wa Waziri  wa Ulinzi na Jeshi la kijenga Taifa Mheshimiwa Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb) Jijini Tanga.
Waziri Tax akipewa ripoti ya Mwendelezo wa Mradi wa Ujeni wa Miundombinu ya Uwanja wa Shule ya Anga ya Kijeshi (SAK) Jijini Tanga, Mhadhara huo ukitolewa na Mwakilishi wa Mkandarasi kutoka SUMAJKT.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad