Serikali Kuendelea Kutafuta Maeneo ya Kihistoria - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, February 25, 2022

Serikali Kuendelea Kutafuta Maeneo ya KihistoriaNa Eliphace Marwa – WUSM, Kilimanjaro

Serikali inaendelea kufuatilia maeneo mbalimbali ya kihistoria nchini kwa lengo la kutunza na kuhifadhi maeneo hayo kwa ajili ya kumbukumbu kwa vizazi vijavyo na kuwa maeneo ya kiutalii wa kiutamaduni.

Akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Kilimajaro, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni toka Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Emmanuel Temu amesema kuwa lengo la Serikali kutambua maeneo hayo ya kihistoria ni kutaka kuyaboresha ili kutunza, kuyalinda na kuyahifadhi.

“ Serikali ina lengo la kuyatambua maeneo mbalimbali ya kihistoria  ili kuweza kuyaboresha kwa ajili ya historia ya nhci yetu kwa vizazi vijavyo na pia itakuwa ni fursa kwa watalii kuja kuayaona na kuongeongeza kipato kwa wananchi wanaozunguka maeneo hayo na nchi kwa ujumla, alisema Dkt. Temu.

Kwa upande wake Afisa Utalii wa Wilaya ya Moshi Vijijini, Bw. Beno Chuwa amesema kuwa mkoa wa wa Kilimanjaro una maeneo mengi sana ya kihistoria ambayo kwa mkakati wa Serikali wa kuyatambua kwa lengo la kuyaboresha utaongeza kipato kwa wakazi wa mkoa wa Kilimanjaro.

“ Mkoa wa Kilimanjaro una maeneo mengi sana ya kihistoria mbali na hili soko la watumwa la Kolila hapa wilaya ya Moshi vijijini, kwa mkakati huu wa serikali wa kuyatambua maeneo haya nina imani utasaidia kutunza kumbukumbu ya nchi yetu na pia kiongeza kipato kwa wananchi wa mkoa wa Kilimanjaro kupitia sekta ya utalii, alisema Bw. Chuwa.

Ziara hii ya Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni mkoani Kilimanjaro ni utekelezaji wa maagizo ya Mheshimiwa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan wa kutaka maeneo hayo kutambulika na kuhifadhiwa kwa lengo la kuwa na utalii wa kiutamaduni.

Katika ziara hiyo mkoani Kilimanjaro, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni, Dkt. Temu aliambatana na Maafisa toka Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja na Maafisa toka Wizara ya Maliasili na Utamaduni.

Jengo lililotumika na wakoloni wa Kijerumani kama ofisa za Posta wakati wa ukoloni lililopo kilila walaya ya Moshi Vijijini mkoani Kilimanjaro.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni toka Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Emmanuel Temu (kulia) akizungumza na Afisa Utalii wilaya ya Moshi Vijijini Bw. Beno Chuwa (kushoto) wakati wa Ziara ya Mkurugenzi huyo Mkoani Kilimanjaro ya kukagua maeneo mbalimbali ya kihistoria nchini, katikati na Afisa Utamaduni toka wizara hiyo Bi. Lilian shayo.
Jengo la kanisa lililotumiwa na Wajerumani wakati wa ukoloni lililopo Kolila wilaya Moshi Vijijini Mkoani Kilimanjaro.
Kaburi la Maaskari wa Kijerumani waliozikwa hapo wakati wa ukoloni lililopo Kolila wilaya ya Moshi vijijini mkoani Kilimanjaro.

Jengo lilotumiwa na wakoloni wa kiarabu wakati wa biashara ya utumwa  lililopo Kolila wilaya ya Moshi vijijini Mkoani Kilimanjaro.
Jengo lilotumiwa na wakoloni wa Kijerumani kama ngome yao wakati wa kipindi cha ukoloni ambalo kwa sasa limeboreshwa na kuwa ofisi za wilaya ya Moshi vijijini mkoani Kilimanjaro.

Picha na Eliphace Marwa – WUSM, Kilimanjaro


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad