HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, February 8, 2022

CCM KILOLO WAIKUBALI KAZI INAYOFANYWA NA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN

 Mwenyekiti wa halmshauri ya wilaya ya Kilolo NNA MPONELA MSOLLA akiwa anafanya usafi katika jengo linalojengw kuwa ofisi ya wilaya ya kilolo.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kilolo Kiliani Myenzi akiwa sambamba na mwenyekiti wa wazazi pamoja na katibu wa vijana katika eneo la jenzi wa ofisi ya chama cha mapinduzi wilaya ya kilolo ambapo wamepania kujenga ofisi ya kisasa kuliko ofisi zote wilaya za chama hicho Tanzania nzima.


katibu wa Itikadi na uenezi wilaya ya kilolo akiwa anafanya usafi katika jengo linalojengw kuwa ofisi ya wilaya ya kilolo.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kilolo Kiliani Myenzi akiwa sambamba na mwananachama wa chama hicho wakipanda mti kwenye eneo la ujenzi wa ofisi mpya za ccm kilolo.
katibu wa Itikadi na uenezi wilaya ya kilolo akiwa anapanda mti kwenye eneo la ujenzi wa ofisi mpya za ccm kilolo
Na Fredy Mgunda,Iringa.
CHAMA cha mapinduzi Wilaya ya Kilolo Mkoani Iringa kimeipongeza Serikali ya awamu ya sita kwa kufanikisha miradi mikubwa ya maendeleo ikiwemo ya Maji uboreshwaji wa miundombinu ya barabara, Afya na elimu.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kilolo Kiliani Myenzi alisema Serikali imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutekeleza kwa vitendo ahadi za maendeleo kwa wananchi ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani na kuchochea maendeleo.

Kiliani Myenzi ameyasema hayo wakati wa hafla ya maadhimisho ya miaka 45 ya CCM wilayani humo na kuwahimiza wananchi kuendelea kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuboresha maisha ya watanzania kupitia miradi ya maendeleo.

Alisema kwa kipindi kifupi ambacho Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ameingia madarakani amefanikiwa kuboresha kila sekta kwa ajili ya kukuza uchumi wa wananchi na kuiletea maendeleo wanananchi.

Myenzi alisema kuwa wananchi wa wilaya ya kilolo mkoani Iringa wanamuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kazi anazozifanya na wapo tayari kumpigania tena mwaka 2025 kwenye uchaguzi mkuu.

Aliesma kwa upande wa wilaya ya Kilolo amepeleka fedha nyingi kutatua kero ya ya Maji uboreshwaji wa miundombinu ya barabara, Afya na elimu na sasa wananchi wanafura na uongozi wake.

Nao baadhi ya wananchama wa chama cha mapinduzi wilaya ya Kilolo walisema kuwa wanaunga mkono kinachofanywa na mwenyekiti wa chama hicho ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya ya keleta maendeleo kwa watanzania.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad