Meneja
Mwandamizi wa wateja Binafsi wa Benki ya NMB, Ali Ngingite akizungumza
wakati wa kuchezesha droo ya kwanza ya kampeni ya MastaBata Kivyakovyako
iliyochezeshwa Dar es Salaam. kutoka kushoto ni Meneja Mwandamizi
kitengo cha kadi, Manfred Kayala, Msimamizi kutoka Bodi ya Michezo ya
kubahatisha, Joram Mtafya


Afisa
Msimamizi Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Samwel Kimaro
(kulia) akimuelimisha mfanyabiashara wa duka la wino wa printa leo
06/01/2022 sokoni Kariakoo jijini Dar es Salaam kuhusu utunzaji wa
kumbukumbu za biashara na utoaji sahihi wa risiti za EFD wakati wa
kampeni ya matumizi ya mashine za EFD sokoni hapo.
**************************
Na Mwandishi Wetu
Wateja
100 wa kwanza wa kampeni ya NMB MastaBata-Kivyako Vyako walipatikana
jana nakuzawadiwa pesa taslimu TZS 100,000 kila mmoja nataasisi hiyo
kiongozi wa shughuli za kifedha nchini.
Washindi hao wamezawadiwa jumla ya TZS milioni 10.
Promosheni
ya MastaBata-Kivyako Vyako ilizinduliwarasmi katikati ya mwezi Disemba
mwaka jana kwa lengola kuchagiza matumizi ya kadi za malipo za
Mastercardkama sehemu ya mchango wa NMB katika juhudi zataifa za kujenga
uchumi usiotegemea sana fedhataslimu.
NMB
pia inatumia kampeni hii ya kuendeleza uchumi wakidijitali kurudisha
fadhila kwa wateja wake waaminifuambao wamekuwa ni muhili muhimu wa
safari yake yamabadiliko ya kidijitali.
Akizungumza
wakati wa droo ya kuwapata washindi wakwanza wa MastaBata-Kivyako
Vyako, MenejaMwandamizi wa Wateja Binafsi wa NMB, Bw. Ali Ngingite,
alisema zaidi ya TZS milioni 200 zitanyakuliwakwenye kampeni hii ya
miezi mitatu.
“Hili
ni toleo la tatu la kampeni za MastaBata zilizoanzarasmi mwaka 2018
kuwahamasisha wateja na wasiowateja wa Benki ya NMB kutumia kadi za
Mastercardwanapofanya malipo na miamala kupitia intaneti,” mtaalumu huyo
wa mikopo binafsi alisema.
“Kama
watangulizi wake, promosheni ya MastaBata-Kivyako Vyako pia ina lengo
la kuwatambua nakuwazawadia wateja wetu waaminifu kwa kuendeleakutumia
huduma zetu,” Bw Ngingite aliongeza nakutabainisha kuwa zitakuwepo pia
droo za kila mwezi naile kubwa ya mwisho.
Wakati
washindi 100 wa kila wiki watashinda TZS 100,000 kila mmoja, 25
watanyakua TZS 1,000,000 kilamwezi na 30 wa mwisho watashinda jumla ya
TZS milioni 90 zikiwa ni TZS milioni kwa kila mshindi.
Bw
Ngingite alisema takribani wateja 1,000 wanategemewa kushinda zawadi za
promosheni yaMastaBata-Kivyako Vyako iliyopangwa kufikia tamatimwezi
Machi.
Kampeni
hii inawahusisha pia wateja wa benki hiyowanaofanya malipo kwa NMB
MasterPass QR. Kama kawaida droo ya jana ilisimamiwa na ofisa
mwandamiziwa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT).
NMB
inasema kampeni zake za MastaBatazimefanikiwa sana kuchagiza malipo ya
kidijitali nchinina matumizi ya kadi za Mastercard kufanya malipo
namiamala mbali mbali.
Mwezi
Novemba mwaka jana, kampuni ya MastercardInternational iliitunuku NMB
tuzo maalumu ya kuwabengi kiongozi wa kuhamasisha matumizi ya kadi
zakenchini.
No comments:
Post a Comment