Mbunge wa Babati Vijijini awakumbuka wenye ulemavu,agawa Vyerehani - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, January 18, 2022

Mbunge wa Babati Vijijini awakumbuka wenye ulemavu,agawa Vyerehani

 

Mbunge wa Jimbo la Babati Vijini mheshimiwa Daniel Sillo akiwa katika picha ya pamoja na wanakikundi hao mara baada ya zoezi la kukabidhi Vyerehani hivyo zinazolenga kuwawezesha katika shughuli za kujikwamua kiuchumi.
Mbunge wa Jimbo la Babati Vijini mheshimiwa Daniel Sillo akisalimiana na mmoja ya watu wenye ulemavu katika kijiji cha Galapo wilayani Babati baada ya kugawa vyerehani kwenye vikundi vya watu wenye ulemavu kwa lengo la kuwawezesha kujikwamua kiuchumi.

Na John Walter-Babati
Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini Daniel Sillo ameendelea kutimiza ahadi ya kutoa vyerehani vya kisasa kwenye vikundi vya wenye ulemavu wa viungo katika kata ya Galapo na Mamire ili kuwasaidia kuweza kujiajiri wao wenyewe.


Mbunge huyo amekabidhi jumla ya Vyerehani tano ikiwa ni ahadi aliyoitoa mwaka 2020 akiwa kwenye kampeni za Mbunge.

Sillo amesema ni muhimu jamii kuwakumbuka watu wenye uhitaji ili nawao waweze kufikia malengo waliyojiwekea kwakua na wao wanaweza kufikia malengo yao endapo watapata ushirikiano.

Aidha amewataka wanufaika kwenda kuzitumia Vyerehani hivyo kwa malengo yaliyokusudiwa ili kuendelea kupunguza baadhi ya changamoto zinazowakabili.

Kwa upende wa wanufaika wa wamemshukuru Mbunge huyo kwa kuwapatia Vyerehani hizo ambazo zinakwenda kubadili maisha yao kwani zitawawezesha kupata fedha ambazo zitawasaidia kujikwamua.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad