Kamishna Mkuu mpya wa Chama cha Skauti wa Kike Tanzania (Tanzania (Tanzania Girl Guides Association ,TGGA), Mary Richard akiapishwa na Kamishna wa TGGA, Wakili Victoria Mandari kushika wadhifa huo mara baada ya kuchaguliwa kwa kura nyingi katika mkutano huo.
Na Richard Mwaikenda
Mwanasheria Mary Richard amechaguliwa kuwa Kamishna Mkuu wa Chama cha Skauti wa Kike Tanzania (Tanzania Girl Guides Association ,TGGA) katika mkutano Mkuu wa chama uliofanyika jijini Dar Dar es Salaam Desemba 13, 2021.
Mary na viongozi wengine wapya wa vijana wa TGGA, Mwenyekiti Irene Jeremiah na Katibu Amenciatha Makoko waliapishwa na Kamishna wa chama hicho, Wakili Victoria Mandari.Viongozi hao watahudumu katika nafasi hizo kwa miaka mitatu.
Kamishna Mkuu mpya, Mary amehidi kuendeleza mazuri yote ya uongozi uliopita kuyafikia malengo waliyojiwekea kwa kufuata katiba ya chama hicho pamoja na kuwajengea uwezo vijana wa kike kujitambua na kufanya kazi kwa bidii kuliletea Taifa maendeleo na wao wenyewe.
Viongozi wengine waliochaguliwa ni Kamishna Mkuu Msaidizi, Florentina Bernard na Makamu Mwenyekiti wa TGGA Taifa, Consolatha Shayo. Nafasi ya Mwenyekiti Taifa iko wazi baada ya kutopigiwa kura kutokana kutojitokeza wala kutoa udhuru katika mkutano huo.
Matokeo ya uchaguzi huo yakitangazwa
Katibu Mkuu wa TGGA, Wintapa Luila akitoa pongezi kwa uongozi mpya na shukrani kwa uongozi uliopita kwa ushirikiano walioutoa.
Wanachama wakiwa katika mkutano huo.
PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDAIMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM 0754264203
No comments:
Post a Comment