TANZANIA WATUMIA MAONESHO YA EXPO DUBAI 2020 KUNADI FURSA ZA UWEKEZAJI - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, December 29, 2021

TANZANIA WATUMIA MAONESHO YA EXPO DUBAI 2020 KUNADI FURSA ZA UWEKEZAJI


Pichani ni baadhi ya viongozi  na wafanyabiashara   waliotembelea Banda la Tanzania na kupatiwa taarifa kuhusu fursa za uwekezaji zilizopo; sababu za kuwekeza Tanzania , na namna ambavyo wawekezaji wanahudumiwa kuanzisha uwekezaji wao nchini ndani ya muda mfupi na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa Huduma za Mahala Pamoja  (One Stop Facilitation Centre) kwenye Ofisi za Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC.)
 


Na Mwandishi Wetu, Dubai

WAKATI Maonesho ya Kimtaifa  maarufu kama Expo Dubai 2020 yakiendelea Jijini Dubai, Banda la Tanzania limeendelea kutumia maonesho hayo kunadi fursa mbalimbali za biashara na uwekezaji zilizopo nchini.

Makundi ya wawekezaji na wafanyabiashara wa kada tofauti wamekuwa wakifika katika banda hilo kwa lengo la kuuliza maswali mbalimbali ambapo wamekuwa wakijibu kwa ufasaha huku zikitumika mbinu kadhaa kuhawahamasisha wawekezaji kuja kuwekeza nchini Tanzania.

Katika banda la Tanzania pamoja na wawekezaji pia baadhi ya viongozi na wafanyabiashara wamefika na kupatiwa taarifa kuhusu fursa za uwekezaji; sababu za kuwekeza Tanzania , na namna ambavyo wawekezaji wanavyosaidiwa kuanzisha uwekezaji wao nchini ndani ya muda mfupi na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa Huduma za Mahala Pamoja  (One Stop Facilitation Centre) kwenye Ofisi za Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).

Kwa mujibu wa Maofisa waliopo katika Banda la Tanzania kwenye maonesho hayo wameiambia Michuzi Blog  kwamba miongoni mwa mambo wanayoulizwa ni aina ya  vivutio vya uwekezaji anavyopata mwekezaji na kufafanuliwa kwamba vivutio vinavyotolewa ni vivutio vya uwekezaji vya kikodi na visivyo vya kikodi.

Aidha imeelezwa pia kwamba wadau wenye nia ya kuwekeza Tanzania wamehimizwa kwamba  Kituo cha Uwekezaji Tanzania ndiyo mlango wa kwanza kwa mwekezaji na  kitawasaidia kupata ardhi ya uwekezaji, leseni,vibali na idhini mbalimbali zinazotakiwa kuanzisha mradi husika.

Wawekezaji wamekaribishwa kuwekeza Tanzania huku wakihakikishiwa kwamba tayari nchi ina  miundombinu ya kuwezesha uwekezaji  katika sekta mbalimbali. Miundombinu hiyo ni kama  maji, umeme, barabara, reli, bandari,  viwanja vya ndege na masoko.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad