HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, December 4, 2021

Shemdoe - Wanaofanya kazi za ununuzi na ugavi wasajiliwe na Bodi ya PSPTB

Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) imefanya kongamano la 12 la Mwaka lililowakutanisha wataalam zaidi ya 1200 ikiwa na  lengo la kujadili ubunifu wenye suluhisho katika utekelezaji wa Ununuzi na Ugavi kwa kutambua ushindani na mapinduzi ya Viwanda kwa maendeleo ya Jamii. Kongamano hilo lililoanza Novemba 30 hadi Desemba 03 mwaka 2021.

Akizungumza wakati wa kufunga Kongamono hilo Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Profesa Riziki Shemdoe aliyemwakilisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Ummy Mwalimu amesema wakurugenzi wa mamkala za Serikali za Mitaa kuhakikisha wanafuata ushauri wa Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi ili kuepusha upatikanaji wa hati chafu kwenye Mamlaka hizo hasa kwenye taasisi zote za Serikali.

Amesisitiza kuwa taaluma waliyoisomea iweniya kuleta tija na ufanisi kwenye Miradi ya Serikali hivyo Wataalam hao wanapaswa kuwa na weledi na pia ambao wanaheshimu taaluma yao.

Shemdoe amesema kuna waajiri ambao wanaajiri maafisa Ununuzi na Ugavi ambao hawajasajiliwa na Bodi kuwa wahakikishe wafanyakazi wao wawe wamesajiliwa na Bodi ya PSPTB ili kusaidia pale wanapokutana Wataalam hao kujadiliana masuala yao kwa uhuru na uwazi.

Amezitaka taasisi zote zilizoko chini ya Mamlaka ya Serikali ya Mitaa na zilizochini ya wizara ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI kuhakikisha wataalamu wote ambao wameajiriwa lakini hawajasajiliwa na Bodi ya PSPTB wanasajiliwa haraka kulingana na Sheria iliyoianzisha PSPTB inavyoelekeza.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Profesa Riziki Shemdoe  akizungumza na Wataalam wa Ununuzi na Ugavi pamoja na wafanyakazi wa Bodi hiyo kuhusu namna walivyojipanga kuwasimamia na kuisimamia taaluma hiyo ili kuwa na tija kwenye maendeleo ya Taifa wakati wa kufunga Kongamano la 12 Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi  lililokuwa na kauli mbiu ya  kujadili ubunifu wenye suluhisho katika utekelezaji wa Ununuzi na Ugavi kwa kutambua ushindani na mapinduzi ya Viwanda kwa maendeleo ya Jamii. Kongamano hilo lililoanza Novemba 30 hadi Desemba 03 mwaka 2021.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi(PSPTB) Godfred Mbanyi akizungumza wakati na Wataalam wa Ununuzi na Ugavi pamoja na kumkaribisha mgeni rasmi Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Profesa Riziki Shemdoe aliyemwakilisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Ummy Mwalimu kwa ajili ya kufunga Kongamano la 12 la mwaka la Wataalam wa Ununuzi na Ugavi.
Baadhi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi  wakifuatilia mada kwenye Kongamamo la 12 la wataalam hao lililoanza Novemba 30 hadi Desemba 03 mwaka 2021 likiwa na kauli mbiu ya  kujadili ubunifu wenye suluhisho katika utekelezaji wa Ununuzi na Ugavi kwa kutambua ushindani na mapinduzi ya Viwanda kwa maendeleo ya Jamii. 
Meneja Masoko na Uhusiano kwa Umma ( PSPTB), Shamim Mdee akizungumza jambo kwenye kongamano la 12 la mwaka la Wataalam wa Ununuzi na Ugavi 

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Profesa Riziki Shemdoe akiwa kwenye picha ya pamoja na makundi mbalimbali mara baada ya kufunga Kongamano la 12 la Mwaka la  Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi  lililofanyika jijini Arusha.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad