Tracy Rabi (pichani), mjasiriamali wa Kitanzania anayefundisha Watoto na vijana kuhusu fedha na ujasiriamali amechaguliwa miongoni mwa watoto 100 bora duniani kote wanaofanya vizuri.
Haya yanajiri baada ya Bi Rabi kuandika vitabu 6, kuanzisha kambi ya watoto na vijana na maonyesho ya biashara kwa kushirikiana na benki inayoongoza nchini ya NMB na kutoa mafunzo kwa mamia ya watoto na vijana.
Huu ukiwa ni mpango wa kwanza duniani wa kuwa na watoto mahiri duniani ambao unalenga kutambua vipaji vya vijana, wametoka kutangaza majina ya watoto 100 bora kwa mwaka wa 2022.
Washindi hawa watakuja kusherehekewa hivi karibuni katika hafla kubwa ambayo imepangwa kufanyika huko Dubai mwakani, mwezi wa Februari.
GCPA ni jukwaa lililounganishwa ambalo lina mpango wa kipekee wa kutambua, kuheshimu na kuhimiza vipaji vya vijana chipukizi kutoka nchi mbalimbali duniani kote.
Waratibu tayari wameshatangaza majina 100 ya watoto watakaowania tuzo hizo mwakani. Kwa maelezo zaidi kuhusu GCPA unaweza kupitia katika tovuti ya www.gcpawards.com. Karibu asilimia 97 ya watoto hawana uwezo wa kuonyesha vipaji vyao baada ya kufikia umri wa miaka 15. Hapa ndipo GCPA inapokuja katika kuhakikisha inasaidia wasanii kama hao watoto wazuri kufanya vyema katika ili kuendeleza vipaji vyao.
Vilevile tuzo za GCPA mwaka 2022, zilipokea maelfu ya maombi kwa kupitia mtandao kutoka katika nchi 68 duniani kote. Baada ya kukamilika, kamati ilifanya tathmini ya kina, kamati ya uteuzi imeorodhesha watoto 100 bora ambao wana umri chini ya miaka 15 katika kategori 48 tofauti ambazo ni michezo, elimu, teknolojia, uvumbuzi, unajimu na dansi.
Mshindi wa tuzo hizo anatarajiwa kutangazwa katika hafla itakayofanyika Dubai, Februari mwaka 2022 ambapo atatoka katika orodha ya watoto 100 ambapo tuzo zitakabidhiwa na watu maarufu duniani. Kamati pia inatarajia kuzindua kitabu cha historia ya tuzo hizo ambazo zitajumuisha watoto 100 kutoka katika nchi mbalimbali duniani, na kitakuwepo katika maktaba mbalimbali duniani.
Mtendaji Mkuu wa tuzo za GCPA Prashant Pandey, ametoa habari njema kwa vyombo vya habari kwamba: “Tunayo furaha kubwa kutangaza majina ya watoto watakaowania tuzo za GCPA yaliyopatikana mwaka huu.
“Ninachukua fursa hii kuwashukuru wazazi wa watoto wote walioingia katika tuzo hizo na kuendelea kuonyesha ushirikiano zaidi ili kuhakikisha tunafikia malengo tuliyojiwekea kwani lengo ni kuendeleza vipaji vyao,”.
“Hapo awali, Bi. Tracy Rabi wa Kids Finance with Tracy alisema “Nina furaha kwamba kuna jukwaa kama hili kwa watoto wadogo kama mimi ambao wanalenga kutumia ujuzi tunaopata kwa kuathiri watoto wengine.
Ninatazamia sherehe ya tuzo na pia kupata nafasi ya kuungana na watoto wengine kama mimi.
Tuzo za GCPA zilitangazwa kwa mara ya kwanza mwaka 2017 katika tuzo za Oscar na A. R. Rahman.
Mwaka 2020, tovuti ya tuzo za GCPA ilizinduliwa na Erik Solheim, Mkurugenzi Mtendaji wa Mazingira na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ambapo tuzo hizo zilifanyika Delhi mwaka 2020 mbele ya waheshimiwa kama Dr. Kiran Bedi, Lieutenant na Dr. Kailash Satyarthi.
Mshauri wa GCPA Dr. K Abdul Ghani, ambaye ni maarufu kwa jina la Green Man of India, aliwaambia waandishi wa habari kwamba: “Kupitia mpango huu tunatarajia watoto wengi wataonyesha vipaji vyao na kujitengenezea nafasi ya kupata fursa mbalimbali kwa jamii ulimwenguni,”.
GCPA ina mpango wa kuendeleza vipaji vya vijana ambapo pia kamati inaangalia jinsi ya kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo wadhamini ili kuhakikisha wanafikia malengo ya kupiga hatua zaidi.
No comments:
Post a Comment