HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, December 6, 2021

Ludewa:Ajinyonga mpaka kufa kwa kutotajwa jina lake wakati wa misa ya shukrani kanisani

Na Amiri Kilagalila, Njombe
MKAZI wa mtaa wa Kanisani B uliopo wilaya ya Ludewa mkoani Njombe anaefahamika kwa jina la Raban Razalo (48) amefariki kwa kujinyonga na waya kwa madai ya kutoridhishwa na kitendo cha Padri wa kanisa la Moravian kushindwa kumtaja jina wakati wa misa ya sadaka ya shukrani iliyofanywa na mkewe baada ya mtoto wao wa miaka 10 kupona majeraha ya kuvunjika mguu.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Njombe, Hamis Issa amesema taarifa zilizobainiwa na jeshi hilo ni kwamba mtoto wa familia hiyo mwenye umri wa miaka 10 alivunjika mguu na kupelekea familia kuzunguka katika hospitali tofauti kupata matibu na kisha kupona jambo ambalo limemsukuma mama kwenda kanisani kutoa sadaka ya shukrani ambayo imekuwa chanzo cha kuondoa maisha ya baba wa familia .

“Walivyoenda kutoa sadaka ya shukrani,Padri wa kanisa hilo amemtaja mama wa mtoto peke yake, baba imemletea sintofahamu na matokeo yake baba ameamua kujinyonga kwa kutumia waya wa TTCL

Kamanda Issa ametoa wito kwa viongozi wa dini kuangalia umuhimu wa familia kwa kuwa inaundwa na baba na mama.

“Viongoizi wa dini angalieni umuhimu wa familia,familia ni baba na mama,ukimtaja mmoja matokeo yake ndipo unapopata sintofahamu na maamuzi yasiyo kuwa na tija”amesema kamanda Issa

Aidha ametoa rai kwa wanafamilia kutochukua maamuzi kwa jambo ambalo wamekwazika huku akisikitika kwa familia hiyo kumuuguza mtoto mpaka kupona na baadaye mzazi anafariki.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad