HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, December 2, 2021

KATIBU MKUU OFISI YA WAZIRI MKUU TIXON NZUNDA AWAASA MADAKTARI KUZINGATIA WELEDI NA MAADILI WANAPOTEKELEZA MAJUKUMU YAO YA KAZI

 NA K-VIS BLOG, KHALFAN SAID, MBEYA

KATIBU Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu), Bw. Tixon Nzunda, amewaasa madaktari kuzingatia weledi na maadili  wanapofanya tathmini za ulemavu na magonjwa yatokanayo na kazi (impairment assessment of occupational accident and diseases).

Bw. Nzunda ameyasema hayo jijini Mbeya, wakati akifungua mafunzo ya siku tano ya tathmini za ulemavu na magonjwa yatokanayo na kazi (impairment assessment of occupational accident and diseases) kwa madaktari na watoa huduma za afya wapatao 100 kutoka mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ikiwemo Katavi, Rukwa, Songwe, Mbeya, Ruvuma, Njombe na Iringa 

“Wakati wote mnapaswa kuzingatia misingi mitatu wakati mkitekeleza majukumu yenu, weledi, uadilifu na uwajibikaji,” alisema Bw. Nzunda.

Alisema kosa lolote dogo (any slight error) litakalofanywa katika kazi ya kufanya tathmini ya ulemavu na magonjwa yatokanayo na kazi litapelekea athari katika maisha ya watu, uchumi wa nchi na kuhujumu Mfuko.

Aidha alisema lengo la Serikali la kuanzisha Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi ni kuhakikisha wafanyakazi wanapata Mafao bora tofauti na sheria ya zamani ya fidia kwa wafanyakazi ili kuboresha fidia. 

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. John Mduma alisema katika kuhakikisha Mfuko unafanya jukumu lake kubwa la kutoa fidia kwa wale ambao wanapatwa na majanga kutokana na kazini, Mfuko unazingatia kufanya tathmini zinafanyika kwa usahihi na kwa haraka.

“Hili la usahihi lina maanisha tunahitaji kushirikiana na wenzetu hawa ambao tayari ni wataalamu katika maeneo hayo na hili la uharaka lina maanisha Mfuko hauwezi kuwa na madaktari kila kona ya nchi kwa hiyo tunahitaji madaktari ambao wako kwenye vituo mbalimbali ili kushirikiana nasi katika kuhakikiasha  swala la tathmini linafanywa kwa haraka na hivyo muhusika anapata fidia stahiki na kwa wakati.” Alifafanua Dkt. Mduma.

Alisema Mfuko utaendelea kufanya kazi zake kwa weledi ndiyo maana unaendelea kuwajengea uwezo wataalamu hao wa afya.

“Kuna miongozo ili kuhakikisha  tathmini zinazotolewa na wataalamu hawa zinakuwa na uhakika, zinaaminika na zinatabirika kwa maana kwamba ziko consistent pale ambapo ukifanyiwa tathmini na mtaalamu A na B matokeo yasitofautiane.” Alifafanua.

Dkt. Mduma aliishukuru Ofisi ya Waziri Mkuu na Serikali kwa ujumla  kwa jinsi ambavyo imekuwa ikishirikiana na Mfuko katika kuhakikisha unaendelea kutoa huduma zake kwa ufanisi zaidi.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu), Bw. Tixon Nzunda akiongea na wataalamu wakati wakati wa mafunzo ya tathmini za ulemavu na magonjwa yatokanayo na kazi kwa madaktari na watoa huduma za afya kutoka mikoa ya Nyanda za Juu Kusini jijini Mbeya Novemba 30, 2021. Mafunzo hayo yanaratibiwa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF).

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu), Bw. Tixon Nzunda akitoa hotuba ya ufunguzi rasmi wa mafunzo ya tathmini za ulemavu na magonjwa yatokanayo na kazi kwa madaktari na watoa huduma za afya kutoka mikoa ya Nyanda za Juu Kusini jijini Mbeya Novemba 30, 2021. Mafunzo hayo yanaratibiwa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF). Wengine pichani ni Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma (katikati) na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, Dkt. Abdulsalaam Omar.

Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma, akitoa neno wakati wa mafunzo hayo

Mkuu wa Huduma za Kisheria, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bw. Abraham Siyovelwa, akitoa mada kuhusu Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi.
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, WCF,  Dkt. Abdulsalaam Omar, akifafanua kuhusu mambo ya kuzingatia wakati wa kufanya tathmini.
Mkurugenzi wa Uendeshaji, WCF, Bw. Anselim Peter, akitoa mada kuhusu taratibu za madai ya fidia.
Baadhi ya washiriki wakisikiliza mada wakati wa mafunzo
Baadhi ya washiriki wakisikiliza mada wakati wa mafunzo
Baadhi ya washiriki wakisikiliza mada wakati wa mafunzo
Baadhi ya washiriki wakisikiliza mada wakati wa mafunzo
Baadhi ya washiriki wakisikiliza mada wakati wa mafunzo
Dkt. Martha Chacha kutoka Hospitali ya Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa, akishiriki kwenye mafunzo 
Afisa Tathmini za madai, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. Matilda Rusibamayila, akijibu maswali mbalimbali ya washiriki kuhusu Mafao yatolewayo na Mfuko
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano, WCF, Bi. Laura Kunenge, (kulia) Mwenyekiti wa jopo la wataalamu (watoa mada), Dkt. Robert Mhina (katikati), na Mtaalamu wa magonjwa yatokanayo na kazi, Dkt. Hussein Mwanga wakijadiliana jambo.
Afisa kutoka WCF, Bi. Innosencia, akiwapatia washiriki vitendea kazi
Washiriki kutoka Mkoa wa Rukwa wakiwa katika picha ya pamoja na meza kuu.
Washiriki kutoka Mkoa wa Ruvuma wakiwa katika picha ya pamoja na meza kuu.
Washiriki kutoka Mkoa wa Katavi wakiwa katika picha ya pamoja na meza kuu.
Washiriki kutoka Mkoa wa Njombe wakiwa katika picha ya pamoja na meza kuu.
Washiriki kutoka Mkoa wa Iringa wakiwa katika picha ya pamoja na meza kuu.
Washiriki kutoka jiji la Mbeya wakiwa katika picha ya pamoja na meza kuu.
Wawezeshaji na Sekretariati ya WCF wakiwa katika picha ya pamoja na meza kuu.
Daktari bingwa wa mifupa na mishipa, Robert Mhina (katikati) akitoa elimu ya jinsi ya kufanya tathmini ya ulemavu ambao mfanyakazi amepata baada ya kuumia akiwa kazini. Hii ni sehemu ya mafunzo kwa madaktari na watoa huduma za afya yaliyoandaliwa na WCF.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad