Tabasamu na Airtel TUNAKUJALI’ Kunufaisha mikoa 12
Kampuni
ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania kupitia mpango wake wa Airtel
TUNAKUJALI leo imetangaza kuzindua kampeni maalum ili kuendeleza
jitihada zake za kusaidia jamii kwa kipindi hiki cha msimu wa sikukuu
ambayo inalenga kuwanufaisha watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu.
Kampeni hiyo itajulikana kama ‘Tabasamu na Airtel TUNAKUJALI’, kupitia
kampeni hiyo itanufaisha mikoa 12 kwa kugusa vituo 12 vinavyolelea
watoto nchini ili kuwapa tabasamu kwa kipindi hiki cha sikukuu za
Krismas na Mwaka
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa
kutangaza kuzindua kampeini hiyo ya ‘Tabasamu na Airtel TUNAKUJALI’,
Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania Beatrice Singano alisema,
“katika msimu huu wa sikukuu tendo hili ni moja ya njia yetu ya
kuonyesha upendo kwa watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu, tumewiwa
kuwafanya watabasamu, kuwaonesha tunawajali na kuwapa matumaini ya
baadae, kwa msimu huu wa sikukuu tunawapa hiki kidogo kwa upendo ili na
wao waweze kusherehekea sikukuu ya Krismas na Mwaka Mpya. Tutaoa msaada
kwenye vituo 12 vya watoto vilivyopo katika mikoa ya Rukwa, Katavi,
Kigoma, Lindi, Kagera, Mtwara, Singida, Dodoma, Dar es Salaam, Mwanza na
Mbeya.
Singano aliongeza, “Furaha ya Airtel siku zote imekuwa
ni kuwa sababu ya kubadilisha maisha ya wengine kupitia miradi mbali
mbali kama Airtel TUNAKUJALI Tunaamini katika dhana ya jamii iliyo sawa
na ndio sababu tumechangua msimu huu wa sikukuu kuishi na hawa watoto”.
Singano
aliongeza kuwa kwa muda mrefu, Airtel Tanzania imekuwa ikifanya miradi
mbali mbali ya kusaidia jamii kwenye afya na elimu. Mradi wetu wa Airtel
Tunakujali ulizinduliwa mnamo 2014 kwa kwa kuwashirikisha wafanyakazi
wa Airtel kuwa na utamaduni wa kusaidia jamii yetu na wamefanya hivyo.
Airtel TUNAKUJALI imekuwa ni chachu kubwa katika kutuunganisha sisi
Airtel na jamii. Sisi Airtel tunaendelea kusaidia jamii inayotuzunguka
kama moja ya njia ya mafanikio yetu, Singano alisema.
Vituo hivyo 12 kila moja itapata zawadi ya Krismas na Mwaka Mpya ya Tzs 2 milioni.
Kwa
uapande wake Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mheshimiwa Godwin Gondwe
ambaye alizindua kampeni hiyo ya ‘Tabasamu na Airtel TUNAKUJALI’
aliwashukuru Airtel kwa kusaidia watoto hasa hasa kwa kuwakumbuka
wanaoishi kwenye mazingira magumu kwa kipindi hiki cha msimu wa sikukuu.
‘’Natambua kuwa kampuni ya Airtel Tanzania inamilikiwa na
serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa asilimia 49 na nina
uhakika chini ya umiliki mpya, Airtel itaendelea sio kuwekeza tu kwenye
masuala ya kusaidia jamii lakini pia upanuzi wa mtandao kitu ambacho ni
lazima tukipongeze’, Gongwe alisema.
Nimepewa taarifa kuwa
Airtel Tanzania kwenye kusaidia jamii imeshirikiana na serekali kwenye
ujenzi wa Hospitali ya Uhuru jijini Dodoma kwa kutoa zaidi ya shilingi
bilioni 2. Ujenzi wa hospitali hiyo unaendelea na ukikamilika itakuwa ni
moja ya hospitali kubwa, yakisasa kwenye ukanda huo. Bado naendelea
kushuhudia Airtel ikiendelea kurudisha kwa kusaidia jamii mnayoihudumia,
leo hii nashuhudia ‘Tabasamu na Airtel TUNAKUJALI’ ambayo imekuja
wakati muafaka ambapo marafiki na wanafamilia wakisherehekea na watoto
wetu hawa watasherehekea pia. Nawapongeza sana na nawaomba muendelee
kusaidia jamii na hasa watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu, Gondwe
aliongeza.
Nae mmoja kati ya wa kituo cha watoto wanaoishi
kwenye changamoto cha Sinza Ijango ambao ni kati ya wafaidika wa
kampeini ya "Tabasamu na Airtel’ TUNAKUJALI, Latifa Mahmoud alisema kuwa
ni muhimu jamii itambue na kupongeza juhudi kubwa zinazofanywa na
makampuni binafsi kama Airtel ya kusaidia jamii ambayo inaishi kwenye
mazingira magumu.
Aliongeza, “Msaada wenu umekuja kwenye muda
muafaka kwani sisi watoto tanaoishi kwenye vituo hivi wanahitaji
kusherehekea kama wengine. Kwa kweli tunashukuru sana na tunaomba
muendelee na moyo huo huo wa kuasaidia wengine.
Mkuu
wa Wilaya ya Kinondoni Godwin Gondwe (kulia) akimkabidhi Mwakilishi wa
Kituo Cha Yatima cha Sinza Ijango cha jijini Dar es Salaam baadhi ya
msaada uliotelewa na kampuni ya Airtel Tanzania kwa vituo 12 vya watoto
yatima ikiwa ni ishara ya kuonyesha upendo kwa kipindi hiki cha msimu wa
sikukuu. Airtel Tanzania kupitia mpango wake wa Airtel TUNAKUJALI leo
imetangaza kuzindua kampeni maalum ili kuendeleza jitihada zake za
kusaidia jamii kwa kipindi hiki cha msimu wa sikukuu ambayo inalenga
kuwanufaisha watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu. Kampeni hiyo
itajulikana kama ‘Tabasamu na Airtel TUNAKUJALI’. Kushoto ni Mkurugenzi
wa Mawasiliano Airtel Tanzania Beatrice Singano.
No comments:
Post a Comment