WAJUMBE WA BODI MENEJIMENTI NA WAFANYAKAZI WA TUZ WAZURU TCRA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, November 18, 2021

WAJUMBE WA BODI MENEJIMENTI NA WAFANYAKAZI WA TUZ WAZURU TCRA

Mkuu wa Kitengo cha Leseni katika Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi Andrew Kisaka akifafanua jambo kwa wajumbe wa Bodi, Menejimenti na Wafanyakazi wa Tume ya Utangazaji Zanzibar (TUZ) waliofanya ziara ya mafunzo ofisi za TCRA kupata uelewa wa namna Mamlaka hiyo inavyosimamia sekta ya mawasiliano Tanzania. 

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Jabiri Bakari akifafanua jambo mbele ya wajumbe wa Bodi, Menejimenti na Wafanyakazi wa Tume ya Utangazaji Zanzibar (TUZ) waliozuru ofisi za Mamlaka kwa lengo la kujifunza namna TCRA inavyosimamia mawasiliano. Katika ziara hiyo TCRA na TUZ wameashiria nia ya kuhuisha baadhi ya vipengele vya mashirikiano baina ya taasisi hizo mbili kwa lengo la kuboresha huduma wanazosimamia.
Mkuu wa Kitengo cha Leseni katika Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi Andrew Kisaka akifafanua ukuaji wa teknolojia ya utangazaji katika kipindi cha Miaka Sitini ya Uhuru wa Tanzania katika Makumbusho ya Mawasiliano mbele ya wajumbe wa Bodi, Menejimenti na Wafanyakazi wa Tume ya Utangazaji Zanzibar (TUZ) walifanya ziara ya mafunzo kujifunza namna TCRA inavyosimamia sekta ya mawasiliano Tanzania.
Mhifadhi wa Makumbusho ya Mawasiliano inayosimamiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bi. Jasmine Kiyungi akifafanua ukuaji wa sekta ya mawasiliano mbele ya Wajumbe wa Bodi, Menejimenti na Wafanyakazi wa Tume ya Utangazaji Zanzibar waliozuru TCRA kujifunza namna mawasiliano yanavyosimamiwa. TUZ imeweka bayana dhamira yake kuboresha zaidi huduma zake mara baada ya ziara hiyo ya mafunzo.
Mhandisi Mwandamizi wa Masafa katika Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw. Victor Kweka akitoa wasilisho mbele ya Wajumbe wa Bodi, Menejimenti na Wafanyakazi wa Tume ya Utangazaji Zanzibar (TUZ) waliozu­ru ofisi za TCRA Makao Makuu kwa ziara ya mafunzo. TUZ imebainisha kuboresha zaidi utoaji huduma za mawasiliano Zanzibar baada ya ziara hiyo ikiwemo maandalizi ya kupokea mabadiliko ya TEHAMA katika kuboresha sekta ya mawasiliano Zanzibar. 
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Jabiri Bakari (wa pili kulia) katika picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi, Menejimenti na Wafanyakazi wa Tume ya Utangazaji Zanzibar (TUZ) waliozuru ofisi za Mamlaka kwa lengo la kujifunza namna TCRA inavyosimamia mawasiliano. Katika ziara hiyo wamepata ufafanuzi juu ya mfumo wa ugawaji na usimamizi wa masafa, utangazaji na utoaji wa leseni za mawasiliano.
Picha na: TCRA

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad