Na Mwamvua Mwinyi, Bagamoyo
VIONGOZI wa umma wametakiwa kuwasilisha matamko ya Mali zao ambapo mwisho wa kuwasilisha taarifa hizo ni Desemba 31 mwaka 2021 .
Zoezi
hilo linaelekea ukingoni hivyo atakaeshindwa kuwasilisha taarifa zake
atakuwa amekiuka Sheria ya maadili ambapo hatua za kinidhamu
zitachukuliwa ikiwemo kulipia faini ya sh.milioni moja ,ama kifungo cha
mwaka mmoja jela.
Akielezea
kuhusiana na Sheria ya maadili kwa madiwani wa Halmashauri ya Bagamoyo,
Ofisa wa maadili kutoka sekretariet ya maadili ya viongozi wa Umma
Kanda maalum,Hamad Bakari Hamad alisema ,dirisha la uwasilishaji wa
matamko hayo lilishafunguliwa tangu octoba mwaka uliopita na mwisho wa
kupokea taarifa hizo ni mwishoni mwa mwaka huu.
Alisema
, viongozi hao wanajua taratibu hizo ,yanapatikana katika sekretariet
ya maadili ya viongozi wa Umma ama katika website ,kwa kupakua taarifa
,unajaza kisha wanatakiwa kuthibitisha kwa mwanasheria wa Serikali au
wakili yeyote anayetoka mahakama ya Tanzania.
Hamad alitoa wito kwa viongozi hao wafuate maadili ya utumishi ili kutumikia wananchi kwa maslahi mapana ya Umma.
"Tupo
chini ya ofisi ya Rais, hatupaswi kusema hatua tunazozichukua
,hatupitishi taarifa sehemu nyingine Kwani tunafanya kazi moja kwa moja
na ofisi ya Rais ,Lakini haimaanishi kwamba hatufanyi kazi "alifafanua
Hamad.
Nae
diwani wa kata ya Yombo Muhammed Usinga alisema wamepokea taarifa na
wanashukuru kupata elimu hiyo na kukumbushwa wajibu wao.
Alielezea kwamba,wapo tayari na yeye Ni miongoni mwa watakaokwenda kuwasilisha sehemu ya mali zake na namna alivyozipata.
Diwani
huyo ,Usinga alisema hiyo Ni Sheria ,ambayo imetungwa na wawakilishi
wetu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,hivyo Wana kila sababu
ya kuisimamia na kutekeleza ili kujiepusha na adhabu
No comments:
Post a Comment