HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, November 11, 2021

PSSSF YATOA WITO KWA WANACHAMA NA WANANCHI KUCHANGAMKIA FURSA YA UWEZESHAJI KUMILIKI NYUMBA

 

 

 

Mkurugenzi wa Fedha Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Beatrice Musa-Lupi (kushoto), akimsikiliza Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Dkt. Bernard Kibese wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam Novemba 10, 2021

MFUKO wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma, (PSSSF) umetoa wito kwa Wanachama na Wananchi kwa ujumla kuchangamkia fursa ya huduma ya kuwawezesha kumiliki nyumba kwa kulipa kidogokidogo na hivyo kuboresha maisha yao.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Fedha wa Mfuko huo, Beatrice Musa-Lupi aliyemwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wakati wa ufunguzi rasmi wa Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam Novemba 10, 2021 ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (Anayeshughulikia masuala ya Fedha na Mipango) Mhe. Jamal Kassim.

Akifafanua kuhusu umiliki huo Lupi alisema PSSSF na Benki ya Azania wanayo makubaliano yanayowawezesha wananchama na wananchi kukopa kutoka benki hiyo kupitia mikopo ya makazi yaani (Mortgage loan) ili kununua nyumba na viwanja vinavyomilikiwa na PSSSF kama vile nyumba za makazi za Buyuni jijini Dar es Salaam.

“Tunashirikiana na wenzetu wa benki ya Azania, mwanachama na asiye mwanachama anakaribishwa kwenye banda letu hapa Mnazi Mmoja atakutana na maafisa wa Mfuko ambao wako tayari kutoa huduma na kuwapa elimu kuhusu majukumu ya Mfuko lakini pia elimu ya fedha kuhusu jinsi Mwanachama au Mwananchi atakavyoweza kununua nyumba hizo kupitia mkopo kutoka benki ya Azania kwa masharti nafuu.” Alifafanua Mkurugenzi huyo wa fedha wa PSSSF.

Kama ambavyo kauli mbiu ya Wiki hiyo inavyosema “Boresha Maisha Kupitia Elimu ya Fedha, PSSSF  ni miongoni mwa taasisi za fedha iliyo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu ikiwa na jukumu la Hifadhi ya Jamii.

“Hifadhi ya Jamii ina majukumu mengi ikiwemo Kusajili Wanachama, Kukusanya Michango, Kuwekeza kwa mujibu wa Sheria lakini pia kulipa Mafao mbalimbali kwa Wanachama na kwa kupitia uwekezaji tunaamini elimu tunayoitoa hapa itawawezesha wanachama na wanachi kutambua fursa zilizopo na hivyo kuboresha maisha yao binafsi na hivyo kuchangia pato la taifa.” Alisema

Waziri waNchi Ofisi ya Rais anayeshughulikia Fedha na Mipango, Jamal Kassim Ali (katikati-mwenye miwani)  akipatiwa maelezo kuhusu Hifadhi ya Jamii, alipotembelea banda la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma, (PSSSF) kwenye Maonesho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam Novemba 10, 2021. Maonesho hayo yaliyoanza Novemba 8 yatafikia kilele Novemba 14 lengo kuu likiwa ni kutoa elimu ya huduma za fedha kwa wananchi. Kauli mbiu ya wiki hiyo ni “Boresha Maisha kwa Kupata Elimu ya Fedha”.
Mkurugenzi wa Fedha Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Beatrice Musa-Lupi akitoa elimu kwa Mwanachama aliyefika kwenye banda la PSSSF.
Mkurugenzi wa Fedha Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Beatrice Musa-Lupi (kushoto) kwa kushirikiana na Meneja Uhusiano na Elimu kwa Wanachama wa Mfuko huo, James Mlowe (wapili kushoto) akitoa elimu kwa wanachama waliofika kwenye banda la PSSSF Novemba 10, 2021
Mkurugenzi wa Fedha Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Beatrice Musa-Lupi (kushoto) akiongozana na mmoja wa Maafisa wa PSSSF walio katika banda la Mfuko huo wakati akielekea kwenye eneo la uzinduzi wa Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu, Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Masha Mshomba (kushoto), akimsikiliza Meneja Uhusiano na Elimu kwa Wanachama PSSSF, James Mlowe
Meneja Uhusiano na Elimu kwa Wanachama PSSSF, James Mlowe (kulia) akimsikiliza Mwanasiasa, Mutamwega Mgaywa aliyefika kwenye banda la PSSSF





No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad