HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, November 8, 2021

NHIF:Maendeleo kiuchumi yanahitaji uhakika wa afya za wananchi

 *Wananchi watembelea banda la NHIF kupata huduma mbalimbali ikiwemo elimu ya mfuko huo.

Na Chalila Kibuda,Michuzi Tv
MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umesema maendeleo ya nchi katika ukuaji wa uchumi unahitaji kuwa wananchi wenye afya ya kupata huduma za afya kwa kutumia bima.

Huduma za bima za afya zina mfanya mwananchi kuwa uhakika wa kuzalisha uchumi wake hata kama atapata ugonjwa na anaweza kutibiwa na kurejea katika uzalishaji wake.

Akizungumza katika Maonesho ya wiki ya Huduma za Kifedha katika viwanja vya Mnazi Mmoja Afisa Masoko Mkuu NHIF Luhende Singu amesema kuwa katika maonesho hayo wananchi wanaweza kupata elimu kuhusiana na Mfuko huo .

Amesema kuwa wamekuja na bidhaa za huduma za vifurushi mbalimbali kulingana na mteja anavyohitaji .

Aidha amesema huduma ya bima ya mtoto kadi yake kwa sasa ni miaka 10 ambapo kila mwaka ni kulipia baada ya hapo unakata kadi nyingine.

Wananchi watembelee NHIF waweze kupata huduma katika maonesho hayo kwani hawataweza kujutia kutokana na kujipanga kwao katika kuwahudumia wananchi ili kazi iendelee.
Afisa Masoko Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Luhende Singu akiwahudumia wananchi waliotembelea banda la NHIF  katika maonesho ya wiki ya huduma za kufedha yanayofanyika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Afisa Mtekelezo wa NHIF Tecla Robert akiwapa machapisho ya bima ya mtoto wananchi waliotembelea maoneosho ya wiki ya huduma za Kifedha zinazofanyika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad