Mwandishi Wetu, Morogoro
Wakati
Mkuu wa wilaya Morogoro Mheshimiwa Albert Msando akiipongeza Biko kwa
kuendesha bahati nasibu ya wazi inayotoa ushindi wa urahisi kulinganisha
na michezo mingine ya kubahatisha, aliwataka waendeshaji wa mchezo huo
wa kubahatisha warudishe faida kidogo kwa jamii ili kuhakikisha kuwa
nchi inasonga mbele kwa kutumia fursa hiyo ya michezo ya kubahatisha.
Mheshimiwa
Msando aliyasema hayo ofisini kwake wakati anazungumza na mshindi wa sh
milioni 10, Luka Andrea Lutuli alizoshinda kwenye droo kubwa ya
Jumapili iliyopita, ambapo makabidhiano ya fedha hizo yalifanyika katika
bank ya NBC, Tawi la Morogoro Mjini.
"Tunajua
biko mnafanya mchezo mzuri unaotoa fedha kwa Watanzania wote, wakiwapo
kutoka mkoani kwetu Morogoro na tukiri hatujawahi kusikia biko
inalalamikiwa kuhusu kutotoa zawadi zenu, ila ni vyema pia mkarudisha
faida kwa jamii ili nchi ijivunie zaidi uwapo wenu," Alisema.
Biko
ni mchezo wa kubahatisha unaoongoza kutoa fedha nyingi kwa Watanzania,
ambapo zwadi za papo kwa hapo zinatoka kila sekunde moja kuanzia sh 2500
hadi milioni 5 papo hapo bila kusahau kutoa zawadi ya hadi sh milioni
40 kila Jumapili ambapo mbali na kucheza kwa namba ya Kampuni 505050 na
kumbukumbu 2456, pia watu wanaweza kucheza live kwa kuingia www.biko.co.tz.
Bahati
nasibu ya biko inachezwa kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi kwa
kufanya miamala kuanzia sh 1000 na kuendelea, ambapo baada ya
kuchungulia nafasi kwa www.biko.co.tz,
mchezaji ataweka namba ya simu na fedha kuanzia sh 1000 na kuendelea na
kubonyeza kitufe cha Cheza Sasa ili awahi nafasi za ushindi.
Mkazi
wa Mikumi mkoani Morogoro Luka Andrea Lutuli mwenye kofia na fulana ya
biko akionyesha furaha yake baada ya kupokea fedha zake jumla ya sh
milioni 10 alizoshinda kutoka kwenye bahati nasibu hiyo ya aina yake.
Kushoto kwa mshindi ni Kajala Masanja Balozi wa Biko na kushuhudiwa na
marafiki pamoja na majirani dukani kwa mshindi huyo. Picha na Mpigapicha
wetu.
Mkuu
wa wilaya ya Morogoro Mheshimiwa Albert Msando kushoto akimpongeza
mkazi wa Mikumi mkoani humo Luka Andrea Lutuli katikati kwa kushinda sh
Milioni 10 kutoka kwenye bahati nasibu ya Biko. Makabidhiano hayo
yalifanyika mkoani Morogoro katika tawi la NBC. Mwingine kushoto ni
Kajala Masanja balozi wa mchezo huo wa Biko.
No comments:
Post a Comment