MAKAMU WA KWANZA WA RAIS AFANYA MAZUNGUMZO NA KIONGOZI WA UNICEF - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, November 10, 2021

MAKAMU WA KWANZA WA RAIS AFANYA MAZUNGUMZO NA KIONGOZI WA UNICEF

 

 


MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ipo tayari kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto (UNICEF), kuifanyia mapitio sera ya Maendeleo ya Mtoto Zanzibar, ili iweze kwenda sabamba na  mweleko wa mahiji ya serikali yaliyopo sasa.

Mhe. Othman ameyasema hayo leo Ofisini kwake Migombani mjini Zanzibar alipozungumza na Mwakilishi Mkaazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa Linaloshughulikia Maendeleo ya Mtoto Duniani Bibi Laxmi Bhawani.

Bibi Laxmi alifika  Ofisini kwa Mhe. Othman kwa mazungumzo rasmi yaliyohusu  ushirikiano kwa masuala mbali mbali na Zanzibar, ikiwemo maendeleo ya mtoto, lishe pamoja na suala la utunzaji na hifadhi Mazingira ya Zanzibar.

Aidha amesema kwamba kutokana na mambo mbali mbali yanayojitokeza katika utekelezaji wa  sera hiyo, hivi sasa inahitaji kufanyiwa mapitio  sambamba na kusaidia mpango wa kuimarisha liche ya mtoto katika kujenga mustakbali bora wa maendeleo ya mtoto wa Zanzibar.

Amefahamisha kwamba shirika hilo kwa muda mrefu limekuwa na mchango mkubwa  kuisaidia Zanzibar katika masuala mbali mbali ya maendeleo ya mtoto hasa wenye mahitaji maalum na lishe ambapo   masuala hayo yamepewa umuhimu  mkubwa katika kujenga maendeleo ya  mtoto Zanzibar.

Mhe. Othman amesema katika majadiliano hayo pamoja na mambo mengine pia wamekubaliana kushirikiana  katika kustawishi mahitaji mbali mbali ya watoto wenye mahitaji maalum Zanzibar hasa katika maeneo ambayo yanayonekana kuwa na matatizo zaidi katika ustawi na maendeleo ya mtoto.

Akizungumzia suala la utunzaji wa Mazingira,  amesema kwamba wamekubalia kutumia mbinu za pamoja za utunzaji na uhifadhi wa mazingira ikiwemo suala la taka ii yawe na faida kwa maendeleo ya mtoto na taifa  kwa  kujmla.

Amesema watoto wenye mahitaji maalum hasa katika maeneo kama vile ya Micheweni ambayo yanaonekana  yapo nyuma kwa kuwepo  matatizo mengi zaidi yanayoathiri maendeleo ya mtoto katika ukuaji na uimarishaji wa mfumo wa lishe yatapewa kipaumbele.

Hata hivyo, amesema katika jitihada hizo za pamoja pia mashirikiano yataelekezwa katika utoaji wa elimu zinaohusu mazingira,  maendeleo ya mtoto pamoja na liche bora ili kuwajenga watoto kukua vyema kimwili na kiakili kwa maendeleo ya taifa.

Kwa upande wake Mwakilishi hyo makaazi wa Unisef Laxmi Bhawani amesema kwamba Shirika la UNISEF  lipo tayari kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  katika kusaidia mambo mbali mbali kwa maendeleo ya mtoto na Zanzibar kwa jumla.

Amesesema pia shirika lake litaimarisha mashirikiano ya wadau na jamii katika kukuuza upatikanaji wa lishe bora kwa watoto sambamba na kutoa elimu kujenga mwamko wa jamii kwa matumizi sahihi ya chakula chenye kujenga liche bora kwa watoto.

Amesema kwamba UNISEF  jitiuhada za pamoja kati ya UNISEFU na Zanzibar  yatasaidia kujenga uelewa zaidi kwa jamii na kwamba masuala hayo yamepewa umuhimu wa kipekee katika kusaidiana na Serikali ya Zanzibar kuwajengea mustakabali bora watoto .

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman akizungumza na Mkurugenzi Makazi wa UNICEF Zanzibar  bibi Laxmi Bhawani. Mkurugenzi huyo alifika ofisi za Makamu wa rais jana ofisini kwa makamu migombani mjini zanzibar kwa mazungumzo ya ushirikiano wa masuala mbali mbali yanayohusu maendeleo ya mtoto, lishe na sera ya mtoto Zanzibar.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman akipokea ripoti ya mandeleo ya juhudi za kupinga ukatili na udhalilishaji dhidi ya wanawake na watoto Zanzibafr kutoka kwa Mkurugenzi Makaazi wa UNICEF Zanzibar  bibi Laxmi Bhawani. makabidhiano hayo yamefanyika huko ofisi ya Makamu migombani mjini ZanzibarNo comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad