DAWASA YAJIPANGA KUMALIZA TATIZO LA MAJI KIGAMBONI - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, November 23, 2021

DAWASA YAJIPANGA KUMALIZA TATIZO LA MAJI KIGAMBONI

 

Wakazi wa Kigamboni wanatarajia kupata huduma ya majisafi, salama na kutosheleza ifikapo mwezi Aprili mwaka 2022 kupitia Mradi wa Kisarawe II utakaosaidia kuondoa kero ya Maji katika Kata saba za wilaya ya Kigamboni  kutokana na kuchimba visima na kujenga tenki la maji litakalokuwa linaweza kuhifadhi maji lita Milioni 15. Hii ni kutokana na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (DAWASA) kutenga fedha kwa ajili ya miradi hiyo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari mara ya kumaliza ziara hiyo, Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amemtaka Mkandarasi wa mradi huo Advent Construction Tanzania kubadili mfumo wa kazi kwa kufanya kazi usiku na mchana kwani vifaa vipo na pia wanaweza kuongeza nguvu kazi ili kumaliza mradi huo kwa wakati.

Amesema Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa maelekezo kwa Wizara ya Maji kuhakikisha wananchi wa Dar es Salaam pamoja na Tanzania kwa ujumla wanapata majisafi na Salama ili kuweza kufikia lengo la kumtua mama ndoo kichwani inatimia.

Pia Aweso amewaomba viongozi wa dini kuendelea na maombi ili mvua ziweze kunyesha zenye manufaa na zisiwe na maafa ili kuweza kurudi kwenye hali ya kawaida ya kuzalisha maji zaidi ya lita milioni 520 maana kipindi hiki nicha mpito.

Pia Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Fatma Almasi Nyangasa amesema uongozi wa wilaya ya hiyo wanafuatilia kwa karibu na makini kwenye usimamizi wa mradi wa maji wa Kisarawe II wanashirikiana na DAWASA ili kuweza kuwapatia wananchi wa wilaya hiyo majisafi na salama.

Naye Afisa Mtendaji Mkuu DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema mradi wa Maji Kisarawe II unahusisha uendelezaji wa visima kumi na mbili vya maji vyenye uwezo wa kuzalisha maji lita milioni 57.

“Mradi huu unatekelezwa kwa sehemu mbili, sehemu ya kwanza ni ujenzi wa kituo cha kusukuma maji, kituo cha kupokea Maji, ulazaji wa mabomba ya maji na ujenzi wa tanki kubwa la kuhifadhi maji la lita milioni kumi na tano linalojengwa Kigamboni na awamu ya pili ikihusisha kazi ya kufunga njia za umeme kwenye visima na kutoa maji kwenye visima na kupeleka kwenye kituo cha kusukuma maji amesema Luhemeja.

Luhemeja  amesema Mradi huu ulianza kutekelezwa mwezi Disemba mwaka 2019 na unatarajiwa kukamilika mwezi Aprili mwaka 2022, huku ukigharimu kiasi cha bilioni 24 fedha za ndani za Mamlaka na kukamilika kwakwe kutanufaisha wakazi 250,000 wa maeneo ya Kibada, Mjimwema, Masonga, Kimbiji, Mpera na maeneo ya karibu.

Mkurugenzi wa Miundombinu na Uwekezaji DAWASA Mhandisi Ramadhani Mtindasi akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Maji, Jumaa Aweso pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe Fatma Almasi Nyangasa kuhusu mradi wa maji wa Kigamboni utakavyoweza kuhudumia kata 7 za Kigamboni wakati wa ziara yake iliyofanyika kwenye mradi wa Ujenzi wa Tanki la maji Kigamboni
Afisa Mtendaji Mkuu DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja akitoa maelezo kwa Waziri wa Maji, Jumaa Aweso pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe Fatma Almasi Nyangasa kuhusu ujenzi wa tenki la kuhufadhia maji linalojengwa Kigamboni wakati wa ziara ya kukagua ujenzi wa mradi huo leo katika wilaya Kigamboni jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Maji, Jumaa Aweso akizungumza na waandishi wa habari kuhusu serikali ilivyojipanga kusimamia miradi ya maji hasa kwa mkoa wa Dar es Salaam kwa kipindi hiki cha upungufu wa maji katika Mto Ruvu wakati wa ziara yake ya kukagua mradi wa maji wa Kigamboni utakavyoweza kuhudumia kata 7 za Kigamboni.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe Fatma Almasi Nyangasa akizungumza kuhusu namna waliya ya Kigamboni watakavyoweza kusimamia mradi ili kuweza kuondoa adha ya upatikanaji wa maji katika wilaya hiyo leo wakati wa ziara ya Waziri wa Maji, Jumaa Aweso  ya kukagua mradi wa maji wa Kigamboni leo jijini Dar es Salaam.  Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja
Afisa Mtendaji Mkuu DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza na waandishi wa habari kuhusu wanavyosimamia mradi wa Ujenzi wa Tanki la kuhufadhia maji litakalokuwa  na ujazo wa milioni 15 ulipofikia wakati wakati wa ziara ya Waziri wa Maji, Jumaa Aweso  ya kukagua mradi wa maji wa Kigamboni leo jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe Fatma Almasi Nyangasa wakikagua ujenzi wa tenki la kuhufadhia maji litakalokuwa  na ujazo wa milioni 15 za maji kutoka kwenye visima mbalimbali vilivyochimbwa katika Wilaya ya Kigamboni mkoani Dar es Salaam.
Mafundi wakiendelea na ujenzi
Muonekano wa tenki la kuhufadhia maji litakalokuwa  na ujazo wa milioni 15 lililofikia kwenye ujenzi.No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad