AIRTEL WABORESHA HUDUMA ZA USAFIRI WA ANGA KUPITIA PRECISIONAIR - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, November 3, 2021

AIRTEL WABORESHA HUDUMA ZA USAFIRI WA ANGA KUPITIA PRECISIONAIR

Mkurugenzi wa Airtel Money Isaack Nchunda akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa kutangaza ushirikiano baina ya Airtel Tanzania na Precision Air ambapo kwa sasa wateja watapata punguzo la hadi asilimia tano wanapolipia tiketi kwa kupitia Airtel Money. Kulia ni Mkurugenzi wa Biashara Precision Air Lillian Masawe.

Mkurugenzi wa Airtel Money Isaack Nchunda (kushoto) na Mkurugenzi wa Biashara Precision Air Lillian Masawe wakionyesha bango baada ya kutangaza ushirikiano mpya ambapo kuanzia sasa wateja wa Airtel watakuwa wanapata punguzo la hadi asilimia 5 pale wanapolipia tiketi kwa kupitia huduma wa Airtel Money.

Na.Khadija Seif, Michuzi Tv
KAMPUNI ya simu za Mkononi ya Airtel imeingia ubia na Kampuni inayotoa huduma za usafiri wa anga nchini PrecisionAir jijini Dar es salaam.

Akizungumza na Waandishi Wahabari wakati wa Uzinduzi huo Mkurugenzi wa Airtel Money, Isack Nchunda amesema ubia huo utaleta urahisi kwa Wateja wa Airtel kufanya Malipo ya tiketi ya usafiri wa anga kutoka kampuni ya Airtel kwenda Shirika la ndege la PrecisionAir.

"Ushirikiano huu ambao tumeingia kati ya Airtel Money pamoja na PrecisionAir utakua wa kipindi hiki cha Msimu wa Sikukuu ambapo Wateja wetu wataweza kufanya uhifadhi wa awali(booking) kwa ajili ya kupata tiketi ya ndege"

Hata hivyo Nchunda ameeleza kuwa ubia huu utakua na Manufaa na utaweza kuwaboreshea huduma wateja wa Airtel pamoja na wasafiri.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Biashara wa Kampuni ya PrecisionAir Lilian Massawe amesema Ushirikiano huo umekuwa wakati muafaka ambapo Shirika lao limejipanga zaidi kuwahudumia Wateja kwa kutoa huduma za usafiri wa anga na kuwa za kipekee.

"Wateja wetu Sasa wanaweza kufanya Malipo ya tiketi zao za ndege kupitia huduma ya Airtel Money,ni sawa na kujihudumia mwenyewe kupitia simu yako ya Mkononi na Mteja anaweza kupokea tiketi ya kielektroniki kupitia simu yake ya Mkononi".

Hata hivyo Massawe amefafanua zaidi kuunga kwa Kampuni hizo mbili pia Wateja watanufaika na 5% pindi watakapofanya Malipo ya tiketi Kupitia huduma ya simu kwa njia ya Airtel Money.

"Wateja wataweza kupata 5% papo hapo watakapofanya Malipo ya tiketi zao na ofa hii itaweza kudumu ya Mwisho mwa mwezi wa disemba na kwa wanaohitaji kufanya safari mwakani wanaweza kuitumia ofa hii mapema kwa ajili ya safari zao."

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad