HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, October 6, 2021

TUTOE HUDUMA INAYOKIDHI MATARAJIO YA WATEJA - MSHOMBA


 

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Masha Mshomba akiongea na wanachama pamoja na wafanyakazi wa NSSF , wakati wa wiki ya Huduma kwa wateja,  Ofisi ya NSSF Mkoa wa Kinondoni.

Meneja wa NSSF Kinondoni, Joseph Fungo akiongea na wanachama pamoja na wafanyakazi wa NSSF, wakati wa wiki ya Huduma kwa wateja,  Ofisi ya NSSF Mkoa wa Kinondoni.

Mwanachama wa NSSF Filbert Magoha akizungumza, wakati alipo fika katika ofisi za NSSF Mkoa wa kinondoni zilizoko Ubungo Plaza Dar es Salaam, wakati  wa wiki ya huduma kwa wateja.

Salha Said Salumu, Mwanachama wa Mfuko wa Taifa wa hifadhi ya Jamii, (NSSF), akizungumza namna alivyopata Mafao yake ya kupoteza  ajira  kwa wakati katika ofisi ya NSSF Mkoa wa kinondoni, wakati  wa wiki ya huduma kwa wateja.

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Masha Mshomba akiongea na wanachama pamoja na wananchi wengine waliokuja kupata huduma ofisi ya NSSF Mkoa wa Kinondoni  , wakati wa wiki ya Huduma kwa wateja.

Mkurugenzi Mkuu wa Clouds Media Group Joseph Kusaga (kushoto) akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Masha Mshomba alipotembelea ofisi za NSSF Mkoa wa kinondoni zilizoko Ubungo Plaza Dar es Salaam, wakati  wa wiki ya huduma kwa wateja. 

Masha Mshomba, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Akikata keki katika kusherehekea  Wiki ya Huduma kwa wateja, NSSF Mkoa wa Kinondoni.

Masha Mshomba, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Akikata keki katika kusherehekea  Wiki ya Huduma kwa wateja, NSSF Mkoa wa Kinondoni.

 

Masha Mshomba (kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Akimlisha  keki Lulu Mengele Meneja Uhusiano na Elimu kwa Umma NSSF, wakati wa wiki ya huduma kwa wateja,ofisi ya NSSF Mkoa wa Kinondoni.

Masha Mshomba (kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Akimlisha  keki Robert Kadege , Meneja wa Huduma kwa wateja NSSF, wakati wa wiki ya huduma kwa wateja,ofisi ya NSSF Mkoa wa Kinondoni.


Masha Mshomba (kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Akimlisha  keki Joseph Fungo, Meneja wa NSSF Kinondoni, wakati wa wiki ya huduma kwa wateja,ofisi ya NSSF Mkoa wa Kinondoni.










Masha Mshomba (kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Akiwalisha keki baadhi ya wanachama na watu mbalimbali waliofika kupata  huduma wakati  wa  wiki ya huduma kwa wateja, NSSF Mkoa wa Kinondoni.

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Masha Mshomba akiongea na wanachama pamoja na wafanyakazi wa NSSF , wakati wa wiki ya Huduma kwa wateja,  Ofisi ya NSSF Mkoa wa Kinondoni.

Salha Said Salumu, Mwanachama wa Mfuko wa Taifa wa hifadhi ya Jamii, (NSSF), akizungumza namna alivyopata Mafao yake ya kupoteza  ajira  kwa wakati katika ofisi ya NSSF Mkoa wa kinondoni, wakati  wa wiki ya huduma kwa wateja.






Masha Mshomba (kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Akiwalisha keki baadhi wawakilishi kutoka Idara mbalimbali katika ofisi ya NSSF  Mkoa wa Kinondoni wakati wa wiki ya huduma kwa wateja.


Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Masha Mshomba Akipokea zawadi kutoka ofisi ya NSSF, Mkoa wa Kinondoni wakati wa wiki ya huduma kwa wateja.

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Masha Mshomba Akipokea zawadi kutoka ofisi ya NSSF, Mkoa wa Kinondoni wakati wa wiki ya huduma kwa wateja.


 

Masha Mshomba Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), akiwa katika picha  ya  pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa NSSF Mkoa wa Kinondoni.



Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

MKURUGENZI Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF,) Masha Mshomba ametoa wito kwa wafanyakazi kuzingatia na kuyaishi maadili ya Mfuko huo ili waweze kufikia malengo ya kutoa huduma bora na endelevu kwa wanachama na wadau.

Mshomba aliyasema hayo leo katika Ofisi za NSSF Mkoa wa Kinondoni wakati wa maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja inayoendekea na iliyobeba kauli mbiu ya;  “Nguvu ya Huduma.” Na kuongeza kuwa wafanyakazi wakizingatia maadili ya NSSF, ni dhahiri kuwa Mfuko utaendelea kukuwa na wateja wataridhika na huduma zinazotolewa.

“Tuhakikishe tunatoa huduma lakini inayokidhi matarajio ya mteja na tutumie nafasi ya kukutana na wateja watueleze  changamoto zipi ambazo wanaona tukizitatua zitaipaisha taasisi yetu." alisema.

Mshomba alisema katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja Mfuko huo umeweka utaratibu kwa baadhi ya viongozi kutembelea ofisi mbalimbali, lengo ni kuona jinsi wanavyotoa huduma kwa wanachama ambazo zitakuwa endelevu.

Alisema katika ofisi ya NSSF Kinondoni alikutana na baadhi ya wanachama akiwemo Joseph Kusaga ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Clouds Media Group ambapo walikuwa na mazungumzo kuhusu uhusiano wa taasisi hizo mbili huku Clouds akiwa miongoni mwa wanachama wa NSSF.

Mshomba alitumia nafasi hiyo kuwahakikishia Watanzania kuwa lengo la NSSF ni kuendelea kuboresha huduma na  wanataka kumfikia mteja aliko katika namna ambayo itampunguzia usumbufu.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Clouds Media Group Joseph Kusaga licha ya kuishukuru NSSF kwa huduma bora wanazotoa kwa wanachama na wadau wao, alibainisha lengo la ziara hiyo ni kuboresha uhusiano uliopo baina yao kwani Mfuko huo ni chombo cha wafanyakazi na umekuwa ukiwahudumia kwa weledi mkubwa.

“Niwapongeze sana NSSF kwa ufuatiliaji mzuri na nina uhakika kuna mambo mengi makubwa ambayo tumeyazungumza yatafanyika kwa  faida ya vijana wa kitanzania na ninawashukuru kwa kuadhimisha wiki hii ya huduma kwa wateja ambayo ni muhimu sana kwa nchi yetu kwa kuangalia huduma zinakwendaje,” alisema Kusaga.

Alisema NSSF inajitahidi sana katika kutoa huduma kwa wanachama na wadau wake na anaamini itaendelea kutoa huduma bora na endelevu kwa vizazi vya sasa na vijavyo.

Vilevile Meneja wa NSSF Kinondoni, Joseph Fungo alisema wanatumia wiki ya huduma kwa wateja kuhakikisha wanaendelea kutoa huduma bora kwa wanachama na kuondoa changamoto zilizokuwepo awali ambazo zilisababisha baadhi ya wanachama kulalamikia huduma katika ofisi hiyo.

Salha Saidi Kalembo, mkazi wa Magomeni ambaye ni mwanachama wa NSSF, akitoa ushuhuda wa maboresho ya huduma za NSSF alisema alifungua madai ya mafao ya kupoteza ajira na kuishukuru NSSF kwani alipata mafao yake ndani ya mwezi mmoja.

Pia mwanachama wa NSSF Filbert Magoha, alisema ameridhishwa na huduma zinazotolewa na NSSF na kutoa wito kwa wanachama wengine wenye madai mbalimbali kufika katika ofisi za NSSF nchi mzima ili waweze kuhudumiwa.

 


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad