TIMU YA WATAALAMU YAPIGA KAMBI MRADI WA MAJI WA MAKONDE, NEWALA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, October 1, 2021

TIMU YA WATAALAMU YAPIGA KAMBI MRADI WA MAJI WA MAKONDE, NEWALA

 

Mashine ya kusukuma maji namba moja katika mradi wa maji wa Makonde, Newala ikifunguliwa na wataalamu wa mitambo tayari kwa kufanyiwa ukarabati.mkubwa.Timu ya wataalamu wa Wizara ya Maji iliyoundwa na Katibu Mkuu, Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga ikiwa eneo la kazi tayari kwa kuanza kazi ya ukarabati mkubwa katika mradi wa maji wa Makonde, Newala mkoani Mtwara. Timu hiyo inajumuisha wataalamu wabobezi katika mitambo ya kusukuma maji (Pumps) na mfumo wa umeme.

Ukaguzi wa mitambo katika mradi wa maji wa Makonde ukifanyika ambapo ipo mitambo mipya sita itafungwa ili kuongeza nguvu na kuhakikisha maji yanafwafikia wananchi kwa saa 24.

Mtaalamu wa mifumo ya umeme akikagua mfumo wa umeme kubaini kiwango kinachofika katika mtambo katika mradi wa maji wa Makonde.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad