HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, October 14, 2021

TFS WAHAMASISHA WATANZANIA KUTEMBELEA VIVUTIO VYA UTALII IKOLOJIA, MALI KALE, WASIFU JITIHADA ZA RAIS SAMIA

 


Matukio mbalimbali katika picha wakati wanafunzi wa Shule ya sekondari Msimbazi mkoani Dar es Salaam kutembelea vivutio vya utalii wa Ikolojia na Malikale Kaole na Mji Mkongwe wilayani Bagamoyo mkoani Pwani

Na Said Mwishehe, Michuzi TV

WAKALA wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS)imewahimiza wananchi kuwa na utamaduni wa kutembelea vivutio vya Utalii wa Ikolojia na Malikale kwa lengo ni kuwawezesha Watanzania kujifunza na kufurahia vivutio vilivyopo.

Akizungumza leo Oktoba 14,2021 Msaidizi wa Kamanda wa Kanda ya Mashariki Bernadetha Kadala amesema leo ni siku ya kumuenzi Baba wa Taifa Mwalim Julius  Nyerere aliyekuwa mwanzilishi na mhifadhi mkuu katika taifa la Tanzania na enzi za uhai alisisitiza sana kuhusu uhifadhi

"Mwalimu Nyerere aliwahi kusema deni la kukata miti bila kupanda ni deni haramu unawaibia wale ambao hawajazaliwa, hivyo kwa TFS tutaendelea kumuenzi baba wa Taifa kwa kulinda ,kuhifadhi na kupanda misitu,"amesema Kadala wakati akizungumza na wanafunzi wa Sekondari Msimbazi jijini Dar es Salaam pamoja na wananchi wengine waliotembelea Mji Mkongwe na Kaole siku hiyo.

Kuhusu utalii wa mali kale Kadala amesema  ni vema watanzania wakajenga utamaduni wa kutembelea na kujionea historia ya nchi yetu ambayo itawajenga kuwa wazalendo na wenye kujua nchi ilikotoka,iliko inakokwenda hasa utalii wa Ikolojia na Mali kale.

"Pia hii itasaidia kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan katika kuutangaza utalii na kukuzaa uchumi wa Tanzania, kwetu TFS tunajisilia farahi kubwa tunaopoona idadi ya watanzajia wanaotembelea hifadhi ya Mali kale ikiongeza, na ukweli gharama ya viingilio ni ndogo kwani ni Sh 2000 kwa wakubwa na watoto ni Sh.1000.

Aidha mbali ya TFS kuhamasisha jamii kutembelea vivutio vilivyopo,imesisitiza umuhimu wa kurithisha vizazi vilivvyopo na vijavyo kwa kutambua Waziri Maliasili na Utalii Dk.Damas Ndumbaro amekuwa na msemo wake kwamba tumerithi tuwarithishe akiwa na maana ya kuhakikisha maliasili zote za Tanzania zinatunzwa na kuendelezwa.

Kuhusu siku ya kumbukumbu ya Siku ya Mwalimu Nyerere , Kadala amesema katika kuadhimisha siku hiyo TFS kupitia Kamishna wa Uhifadhi TFS Profesa Dos Santos Silayo ambaye ametangaza ofa kutembelea maeneo yote ya utalii na malikale bure kwa siku ya Nyerere Day.

"Hii yote inakuja katika kuunga mkono jitihada za Rais wetu mpendwa katika kuunganza utalii kama ambavyo ametuonesha njia kwa vitendo, Rais Samia ameanza na kuutangaza utalii wetu kimataifa kupitia Royal Tour,"amesema Kadala.

Amefafanua TFS inamiliki hifadhi za mazingira asilia 24 na vituo vya mambo ya kale sita ambavyo ni sehemu nzuri kwa utalii wa ikolojia.Baadhi ya vituo hivyo ni Magofu ya Kaole,Mji Mkongwe, Mapango ya Michoro ya Kondoa Irangi na Tanga Tongoni .Wakati mazingira asilia kuna Pugu Kazimzumbwi, Amani Tanga, Uruguru, pamoja na mashamba ya Miti.

Kwa upande wake Hozmin Hanif ambaye ni Mratibu wa taasisi isiyo ya kiserikali ya Tanzania Youth in Protecting Society ambayo ina Klabu za za uzalendo kwenye shule za sekondari nchini amesema baada ya TFS kutoa ofa ya wananchi kutembelea hifadhi za malikali na utalii ikolojia wameona ni vema wakatumia fursa hiyo kuwapeleka wanafunzi kutembelea vivutio vya malikale vilivyopo Bagamoyo.

Amesema lengo la kuwapeleka wanafunzi hao  ni kufundisha uzalendo na kuhamasisha utalii wa ndani kwa vijana waliopo shule za sekondari

ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 22 ya kifo cha baba wa Taifa na kwamba wao kama wazalendo wanaonesha kuwa wanaenzi na kuyaishi maono ya baba wa Taifa.

Pia wanaunga mkono juhudi za Rais Samia katika kuutangaza utalii ,hivyo wamesharikiana na  TFS kuwaleta watoto kwenye maeneo ya kihistoria na malikale Ili kujenga jamii yenye ari na yenye kupenda na kutunza vilevile kuzitembelea tunu za taifa letu na kizitangaza kimataifa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad