HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, October 18, 2021

Shirika la Interpeace Afrika latoa semina ya mafunzo ya amani kwa Nchi za maziwa makuu (ICGLR)


Washiriki katika mafunzo ya amani na utatuzi wa migogoro kutoka nchi za maziwa makuu (ICGLR) wametakiwa kutoa elimu stahiki juu ya amani na utatuzi wa migogoro kama suluhisho litakalolifanya eneo husika kuwa salama.
Akizungumza katika semina hiyo ya mafunzo ya amani na utatuzi wa migogoro kwa washiriki kutoka nchi hizo, Mwakilishi wa Interpeace katika Nchi za maziwa makuu, Bw. Frank Kayitare amewataka washiriki wa mafunzo hayo kutumia maarifa watakayopata kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa amani na utatuzi wa migogoro kama njia muhimu ya kupata maendeleo.
“Nyinyi ndio mtakao kuwa mabalozi katika kuelimisha jamii katika nchi zetu juu ya umuhimu wa amani na utatuzi wa migogoro jambo ambalo litazifanya nchi tunazotoka kuwa sehemu salama kwa maendeleo ya watu wetu”, alisema Bw. Kayitare
Aidha Bw. Kayitare ameushukuru Umoja wa Ulaya (EU) kwa ufadhiri wao ambao umewezesha kutekeleza mipango ya utoaji wa mafunzo hayo ya amani na usuluhishaji wa migogoro hasa katika ngazi ya kijamii na kuangazia nafasi ya mwanamke kwenye ushiriki wa kuleta amani Afrika.
Alibainisha kuwa matarajiao ya mafunzo hayo ni kuona washiriki hao wakienda kutumika mstari wa mbele kwenye kujenga jamii bora yenye amani na isiyo na migogoro na machafuko.
“Tuna matarajio makubwa na washiriki wetu, na kile tunachokipandikiza kwao kitaenda kuwa na manufaa sio tu kwa ngazi ya jamii bali hata kwenye ngazi ya kitaifa kwenye mataifa yetu tunayotoka”, alisema Bw. Kayitare.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Jinsia, Wanawake na Watoto (ICGLR) Bi Flaviana Charles amesema mafunzo hayo ni sehemu ya mafunzo endelevu ambayo yamekuwa yakitolewa kwa nchi za maziwa makuu yenye lengo la kusaidia kuimarisha amani, jinsia demokrasia katika nchi hizo.
“Huu kwetu ni muendelezo tu, kwa kuwa tumekuwa tukifanya mafunzo hayo na tutaendelea kuyafanya kwa kuwa ni mafunzo muhimu yenye malengo muhimu kwa ustawi wa mataifa yetu”, alisema Bi. Flaviana.
Amesema wanawake na vijana ni makundi muhimu ambayo yakitumiwa vizuri kwenye jamii yatakuwa msaada mkubwa kwenye kuleta amani na kufanya usuluhuhishwaji wa migogoro barani Afrika.
“Kwenye mafunzo haya kuna wanawake na hata vijana, hii inatoa picha nzuri kwa siku za usoni kwa kuwa makundi haya yana ushawishi mkubwa kwenye jamii zetu kwenye kuhamasisha amani na kufanya masuluhisho ya migogoro”, alisema Bi. Flaviana.
Semina hiyo ya mafunzo ya amani nausuluhishi wa migogoro inafanyika nchini kwa siku tatu na kuzipitisha nchi za Rwanda na Jamhuri ya Demokrasia ya Congo kama nchi zitakazo fanyiwa majaribio kutoka na mpango huo wa mafunzo waliyoyatoa kwa lengo la kusulihisha migogoro mbalimbali iliyopo katika jamii.
Mkurugenzi wa Jinsia, Wanawake na Watoto wa Jumuiya ya Nchi za Maziwa Makuu(ICGLR), Dkt. Flaviana Charles, Akizungumza kwenye semina ya siku tatu ya Mafunzo ya Amani na utatuzi wa migogoro katika nchi 12 washiriki wa ukanda wa maziwa makuu inayofanyika Jijini Dar es salaam, lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo washiriki hao kuhusiana masuala ya amani na usuluhishaji wa migogoro katika ngazi ya jmii na wakawe mabalozi wazuri katika Nchi zao.
Mwisho.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad