Na.Vero Ignatus Arusha
Rais wa jamburi ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amemuagiza mkuu wa wa mkoa wa Arusha John Mongela kwenda
 wilaya ya Ngorongoro kuangalia tofati zilizopo Kati ya wananch 
wanaoishi  ndani ya hifadhi  na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ili 
kuangalia namna ya kutatua
Mhe.Rais alisema 
kuwa  huko awali kulikuwa na migogoro mingi Sana, kwani vijiji vingi 
vimeingia kwenye hifadhi ,lakini wakaangalia migogoro hiyo kwa undani 
zaidi ya vijiji 100 wameamua kuviacha vilipo, kwani wakivihamisha hakuna
 pa kuvipeleka
Aidha alimshukuru Leigwanani Kisongo kwa
 kumwambia kwamba Serikali ikikaa pamoja na wafugaji wanaoishi ndani ya 
Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, mgogoro huo utatatulika,hivyo Rais 
wameahidi kumtuma mkuu wa mkoa kutafuta Suluhu.
"Vijiji zaidi ya Mia moja tumeviacha vibakie vilipo ,tukiviahamisha hatuna pa kuvipeleka,Ila nakushukuru Sana Leigwanani Kisongo kwamba
 umetuambia tukikaa na sisi mgogoro utatatuta,nataka nikuahidi namleta 
mkuu wa mkoa aje kukaa na ninyi yakimshinda nitaingia mwenyewe" Alisema 
Rais.
Wakati huohuo Mhe.Rais amempa miezi 3 Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya karatu Rajabu Karia Magara kuhakikisha anakamilisha  ujenzi wa hospital hiyo ili kumaliza tatizo la wqgonjwa kukosa huduma ya matubabu 
 
 Karatu Kuna hospitali ya wilaya ambayo imeanzwa kujengwa kuanzia mwaka 
2019 fedha yote umetolewa ipo pale iqna hospitali haijaisha, nakupa 
miezi mitatu kwasababu fedha yote unayo sioni kwanini hospital haijaisha
 Ina mwaka wa pili Sasa haijaisha"Alisema Mhe.Samia
Amemtaka
 kuhakikisha kuwa  hospitali hiyo inamalizika kwa muda alioutoa ili 
akienda  Karatu nikute imemalizika nije niifungie na wannachi wapate 
huduma 
 tukiviahamisha hatuna mahali pa kuvipeleka
Akizungumza
 juu ya ujenzi wa Stendi Jiji la Arusha Mhe.Rais Alisema kuwa hlmshauri 
Jiji ipeleke mchoro kwani Serikali inamradi wanaandaa wa kuomba fedha 
hivyo zikipatikana watazileta kwaajili ya ujenzi wa Stendi hiyo
Kuhusu
 suala la machinga. Alisema kuwa hawawezi kuruhusu sir za mjini 
kuharibiwa Ila utatafutwa utaratibu Maalum ili kuhakikisha wanpatiwa 
maeneo ya kufanya biashara zao
Kuhusiana
 na masuala ya mikopo kwaajili ya kuinua uchumi alisema kuwa mikopo 
yenye masharti nafuu kwaajili ya manufaa ya Taifa ataiileta Ila mikopo 
kichefuchefu hatoweza kunichukua kwasababu inawasogeza watanzania 
inaleta Maendeleo hivyo hataogopa kuichukua
“Nataka
 kuwaahidi watanzania nitaangalia mikopo yenye unafuu kwa nchi yetu, 
inayoleta faida kwa nchi yetu hiyo nitaichukua, mikopo chechefu 
sitaichukua lakini ile ambayo inaleta nafuu kwa nchi yetu, inatusogeza 
watanzania inaleta maendeleo hiyo sitaogopa nitaichukua,”- Rais Samia 
Suluhu Hassan.
 

 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
No comments:
Post a Comment