HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, October 4, 2021

PROMOSHENI YA NMB 'BONGE LA MPANGO' AWAMU YA PILI HADHARANI TENA ,ZAWADI MILIONI 246 KUMWAGWA KWA WASHINDI

BENKI ya NMB imezindua promosheni yenye lengo la kuwaunganisha wateja wao pamoja na wateja wapya ambayo imepewa jina la 'Bonge la Mpango Awamu ya pili' na kampeni hii itadumu kwa miezi mitatu.

Kampeni hiyo imelenga kuwawezesha wateja wao kushinda fedha taslimu na pikipiki za miguu mitatu maarufu kwa jina la Toyo.

Akizungumzia uzinduzi huo Afisa Mkuu wa wateja binafsi na biashara, Filbert Mponzj amesema Bonge la Mpango Awamu ya pili inakusudia kurejesha faida kwa wateja pamoja na kuhamasisha utamaduni wa kujiwekea akiba kwa Watanzania na hii ikiwa ni mwendelezo wa kampeni ya Bonge la Mpango iliyozinduliwa mwezi Februari.

" Mshindi mmoja wa Toyota Fortuner

Watatu wakajinnyakulia TATA Mid- sized Pick-up almarufu kama Kirikuu

24 walioshinda Lifan 3- wheeler

Na 120 waliwekewa kiwango cha 100,000 hadi 500,000 kwenye akaunti zao.

Kikubwa zaidi, katika kampeni hii, zaidi ya shilingi Milioni 246 zitatumika kutoa zawadi kwa washindi, huu ukiwa ni mkakati wetu kama Benki kwa mwaka 2021 ambapo tunakusudia kuendelea kuifanya NMB kuwa chaguo namba moja kwa usalama wa fedha za wateja, suluhisho za kifedha na kwa faida," Amesema Mponzi.

Amesema wateja wote wa NMB wa sasa na wale watakaofungua akaunti mpya wana nafasi ya kushinda zawadi ya toyo 50 kila moja ikiwa na gharama ya shilingi milioni 4.4.

Pia washindi 120 watajishindia kila mmoja 100,000 jumla ikiwa fedha taslimu shilingi milioni 12.

"Wateja wanaofungua akaunti za NMB kwa mara ya Kwanza, wakaweka kiasi cha shilingi 100,000, au kuhamisha shilingi 100,000 kutoka kwenye benki zingine na hata mitandao mingine ya simu watajishindia zawadi mbalimbali kutoka NMB kila wiki na kila mwezi.

Kwa wale ambao watafungua akaunti ya NMB au wateja wenye akaunti ya NMB na watakaoweka kiwango cha chini cha shilingi 100,000 kwa muda usiopungua mwezi mmoja, watajiongezea nafasi ya kuingia kwenye droo ya finali itakayochezeshwa mwishoni mwa mwezi December ambapo Toyo 14 zenye thamani ya shilingi Milioni 62 zitatolewa," Amesema Mponzi.

Amesema wanatoa fursa kwa wateja wao katika kipindi hiki cha mavuno kwa wateja na watanzania wote kufungua akaunti katika Benki ya NMB ili kuingia kwenye orodha ya washindi na pia kupata fursa ya kutunza akiba kwa njia salama zaidi na NMB.


Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi (katikati), akizindua promosheni ya Bonge la Mpango awamu ya pili, ikiwa na lengo la kuhamashisha nidhamu ya kuweka akiba kwa wateja. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.


Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi (katikati), akizindua promosheni ya Bonge la Mpango awamu ya pili, ikiwa na lengo la kuhamashisha nidhamu ya kuweka akiba kwa wateja. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi (kushoto), akizindua promosheni ya Bonge la Mpango awamu ya pili, ikiwa na lengo la kuhamashisha nidhamu ya kuweka akiba kwa wateja. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki

Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi (kushoto), pamoja na maofisa waandamizi wa benki hiyo wakizindua rasmi promesheni ya Bonge la Mpango awamu ya pili. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.
Miongoni mwa zawadi ya toyo yenye thamani ya shilingi milioni 4.4 ikioneshwa kwenye uzinduzi huo. Jumla ya zawadi za toyo 50 kila moja ikiwa na thamani ya shilingi milioni 4.4 zitatolewa kwa washindi awamu hii.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad