MIRERANI WAFURAHIA WIKI YA NMB HASA HUDUMA YA MIKOPO - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, October 6, 2021

MIRERANI WAFURAHIA WIKI YA NMB HASA HUDUMA YA MIKOPO

 

Na Mwandishi wetu, Mirerani
WADAU wa madini ya Tanzanite wa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wameipongeza Benki ya NMB Kwa kuweka huduma ya mikopo kwa wadau wa madini wakiwemo wafanyabiashara na wachimbaji.

Kaimu ofisa madini Mkazi Mirerani (RMO) Castro Maduwa na Diwani wa Kata ya Mirerani Salome Nelson Mnyawi, wamesema hatua hiyo itaboresha sekta ya uchimbaji wa madini ya Tanzanite.

Kaimu ofisa madini mkazi Mirerani, Castro Maduwa amesema hatua ya kuweka mikopo kwenye zana za ulipuzi kwa wachimbaji wadogo wa madini itawapa nguvu ya kuchimba madini hayo.

Maduwa amesema kulikuwa na changamoto kubwa kwa wachimbaji kukosa mitaji ila kupitia mikopo hiyo watanufaika nao wapo tayari kutoa taarifa sahihi za wachimbaji ili wapate mikopo.

Diwani wa kata ya Mirerani Salome Mnyawi amesema mikopo hiyo nafuu kwa wafanyabiashara wa madini ya Tanzanite na wachimbaji madini itakuwa faraja kwenye sekta hiyo.

Mnyawi amesema japokuwa yeye ana maslahi kwa benki zote kwa sababu ni kiongozi wa kisiasa lakini anafurahishwa na benki ya NMB kwa namna inavyotoa huduma kwa wateja wake.

Ofisa mtendaji mkuu (TEO) wa Mamlaka ya mji mdogo wa Mirerani, Evence Mbogo amesema benki ya NMB imekuwa ikiunga mkono juhudi za maendeleo kwa kutoa misaada kwa jamii.

“Nawapongeza NMB kwa namna mnavyosaidia jamii kupitia madawati kwa wanafunzi wa shule na vifaa tiba kwenye zahanati, vituo vya afya na hospitali mbalimbali,” amesema Mbogo.

Ofisa mtendaji wa kata ya Naisinyai, Valentine Tesha amesema japokuwa amehusika kufanikisha kuwa na taasisi za fedha ikiwemo benki ya NMB kipindi akiwa mtendaji wa kata ya Mirerani ila anaridhishwa na utendaji wa benki hiyo.

“Nilishawishi mameneja wa kanda waanzishe benki Mirerani ili wananchi wa zaidi ya kata 10 wanufaike nazo na NMB mkawa miongoni mwao na sasa mafanikio yenu na utendaji ni asilimia 300,” amesema Tesha.

Katibu wa chama cha wachimbaji madini mkoa wa Manyara, (MAREMA) Tawi la Mirerani, Rachel Njau, amempongeza Meneja wa NMB Tawi la Mirerani Allan Kombe kwa namna anavyoongoza Tawi hilo.

“Meneja huyu hakai ofisini anawafuata watu kwenye shughuli zao na kuwapa elimu mbalimbali juu ya benki namna ya kuhifadhi fedha na kupatiwa mikopo,” amesema Njau.

Meneja wa huduma kwa wateja wa Benki ya NMB Tawi la Mirerani, Athuman Mwaya amesema benki hiyo imezindua maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja kwa kuahidi kuendelea kuwahudumia wateja wake kwa viwango bora ili kudumu katika nafasi yao kama taasisi ya fedha pendwa na inayoongoza nchini.

Amesema hati ya kiapo cha huduma kwa mteja ni nyenzo muhimu katika kuweka uhusiano mzuri na wateja wa benki hiyo ili waendelee kuiamini na iweze kuendeleza ushindani wenye tija sokoni.

“Kauli mbiu ya wiki ya huduma kwa wateja kwa mwaka huu ni ‘Nguvu ya Huduma’ na ili NMB iendelee kuongoza kwenye utoaji huduma kwa wateja, maadhimisho haya tunayatumia kuzindua hati ya kiapo cha huduma kwa mteja kuonyesha kwa vitendo nguvu ya huduma kwa wateja wetu,” amesema Mwaya.

Amesema kimsingi hati hiyo ina ahadi tano za benki kwa mteja ambazo ni kupatikana kwake kwa haraka, usikivu, uhakika na kuaminika, usalama wa taarifa za mteja na weledi na nidhamu.
Picha ya Pamoja
No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad