HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, October 4, 2021

IGP SIRRO AKUTANA IGP WA CONGO NA KUAHIDI KUSHIRIKIANA KUIMARISHA HALI YA USALAMA

 

 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amesema kuwa, shirikisho la Wakuu wa Polisi Mashariki Mwa Afrika (EAPCCO) litaendelea kuimarisha hali ya usalama kwenye nchi za shirikisho hilo kwa kufanya operesheni za pamoja na kuhakikisha wanadhibiti uhalifu unaovuka mipaka na kwa kubadilishana taarifa za uhalifu na wahalifu.

IGP Sirro amesema hayo leo jijini Dar es salaam wakati alipokutana na Mkuu wa Jeshi la Polisi wa nchi ya DRC Congo, IGP Dieudonne Bahigwa ambaye amefanya ziara ya kikazi hapa nchini ikiwa ni siku chache kabla ya kupokea kijiti cha Uwenyekiti wa Shirikisho la Wakuu wa Polisi Mashariki Mwa Afrika lenye jumla ya nchi 14 wananchama wa shirikisho hilo.

Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini DRC CONGO IGP Diedonne Bahigwa, amesema kuwa, ziara yake nchini Tanzania imelenga kujifunza namna ambavyo IGP Sirro alivyofanikiwa kuliongoza shirikisho hilo kwa kipindi cha miaka miwili huku IGP huyo wa Congo akiahidi kuendeleza ushirikiano wa pamoja juu ya kuweza kufuatilia uhalifu unaofanyika kwenye ziwa Tanganyika na maeneo mengine.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad