HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, October 22, 2021

ECOBANK TANZANIA YATOA MSAADA WA NGUO ZA WAGONJWA NA VITI HOSPITALI YA MUHIMBILI

 ECOBANK Tanzania imetoa msaada wa nguo za wagonjwa pamoja na viti kwenye Idara ya Magonjwa ya Afya ya Akili katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ikiwa ni sehemu ya mkakati wa Kampuni ya Ecobank wa kutenga siku maalum kusaidia jamii katika maadhimisho ya uwajibikaji wa kijamii kwa kila mwaka ambayo huzishirikisha jamii zote ndani ya bara la Afrika. Nchi zote 33 Barani Africa zenye benki ya Ecobank zimekuwa zikitenga siku maalumu kila mwaka (Ecobank Day) kusaidia jamani zinazoizunguka ili kutumiza lengo la kurudisha kwa Jamii.

Kwa mwaka huu Maadhimisho ya Siku ya Ecobank yamefanyika  leo tarehe 22 Oktoba yakiwa na kauli mbiu ya ‘Afya ya Akili – Ni Wakati wa Kuzungumza na Kutenda!’ Kaulimbiu hii imelenga hatua ya mwisho ya kampeni ya miaka mitatu ya Ecobank ya kuongeza uelewa na kusaidia kuzuia Magonjwa yasiyoambukiza.

Akizungumza wakati wa kutoa msaada wa Viti na nguo za wagonjwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili  Mkurugenzi Mkuu wa Ecobank Tanzania Bw. Charles Asiedu alisema benki hiyo   imeazimia kuongeza uelewa na kusaidia kuzuia mambo yanayohusiana na  magonjwa ya Afya ya Akili, ambayo yanaweza kumwathiri mtu yeyote.

“Bado kuna dhana nyingi potofu kuhusiana na Afya ya Akili hapa nchini Tanzania. Ni muhimu sana kuzungumza kwa uwazi kuhusiana na Afya ya Akili bila ya kuhisi fedheha au miiko ya kimaadili  na pia tumeitumia siku ya Ecobank 2021 kusambaza taarifa hizi ili ziwafikie watu wengi kadri iwezekanavyo kwasababu sasa ni wakati wa kuzungumza na kutenda kwenye masuala yanayohusu Afya ya Akili” alisema Asiedu

Pia amesema utoaji wa elimu ya afya ya akili kwa wafanyakazi wanashirikiana na  “ARIS Risk and Insurance services” na wametoa msaada wa nguo za wagonjwa na viti katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili katika kitengo cha Afya ya akili.

Naye Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Afya ya Akili katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Dk Frank Masao ameishukuru Ecobank kwa kuweza kuwapatia msaada huo kwani kila mwaka wagonjwa wa Afya ya akili wamekuwa wakiongezeka na kupelekea upungufu wa vifaa vya afya vinavyoweza kusaidia kwenye utoaji wa huduma.

Pia amesema wanaume ndio wanaoongoza kuwa na magonjwa wa Afya ya Akili kwani kwa miaka miwili iliyopita imeonesha kuwa wanaume ni wengi ukilinganisha na wanawake pamoja na uwepo wa Uviko 19 umesababisha wagonjwa wakili kuongezeka kutokana na zuio au uoga wa wananchi kuja kupata matibabu katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Siku ya Ecobank ni tukio la kila mwaka ambalo kwa mara ya kwanza lilifanyika mwaka 2013, likiwa na mrengo wa kufanyika kila mwaka ikibeba kaulimbiu maalumu.  Kaulimbiu hizi zimekuwa zikitoa Elimu kwa Vijana Wadogo Afrika (2013); Kuzuia na Kudhibiti Malaria (2014); kila mtoto wa Kiafrika ana haki ya kuwa na maisha bora ya baadaye (2015); Elimu ya TEHAMA shuleni na kuboeresha Afya ya Uzazi (2016); Usimamizi wa maji salama (2017); Makazi ya yatima  (2018); Saratani (2019); na Ugonjwa wa kisukari (2020).

Mkurugenzi Mkuu wa Ecobank Tanzania Bw. Charles Asiedu akimkabidhi msaada wa nguo za wagonjwa Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Afya ya Akili katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk Frank Masao kwenye hafla iliyofanyika leo katika hospotali hiyo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Ecobank Tanzania Bw. Charles Asiedu akimkabidhi msaada wa viti Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Afya ya Akili katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk Frank Masao kwenye maadhimisho ya siku ya Ecobank iliyofanyika katika hospitali ya Muhimbili leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Ecobank Tanzania Bw. Charles Asiedu akizungumza na uongozi wa  Idara ya Magonjwa ya Afya ya Akili, wafanyakazi wa Ecobank Tanzania, wafanyakazi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kuhusu namna wanavyoitumia siku ya Ecobank katika kusaidia jamii wakiwa na lengo la kurudisha kwa jamii wakati wa kutoa msaada wa wa nguo za wagonjwa na viti uliofanyika katika Idara ya Magonjwa ya Afya ya Akili katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). Kushoto ni Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Afya ya Akili katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk Frank Masao 
Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Afya ya Akili katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk Frank Masao akizungumza na wafanyakazi wa Ecobank Tanzania, wafanyakazi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili pamoja na waandishi wa habari wakati wa kupokea msaada wa nguo za wagonjwa na viti uliofanyika katika Idara ya Magonjwa ya Afya ya Akili katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
Baadhi ya wafanyakazi wa Ecobank Tanzania pamoja na wafanyakazi wa Idara ya Magonjwa ya Afya ya Akili katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) wakifuatilia tukio la kutoa msaada wa nguo za wagonjwa na viti uliofanyika katika Idara ya Magonjwa ya Afya ya Akili katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo jijini Dar es Salaam.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad