HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, September 21, 2021

Rekodi mpya yawekwa Mlima Kilimanjaro

 


*Watalii wacheza Mchezo wa Vikwazo Kreta
*Wateremka hadi chini kwa kukimbia

KUNDI la watalii 45 kutoka mataifa 23 kote duniani limeweka rekodi mpya katika Hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro kwa kufanya michezo ya kupita katika vikwazo kwenye eneo la kreta, pamoja na kushuka kutoka katika kilele cha Uhuru kwa kukimbia.

Watalii wanamichezo hawa waliokuwa wakishiriki katika zoezi maalum la kuruka vikwazo kwenye maeneo yenye miinuko ya juu waligawanyika katika makundi makuu mawili kwenye zoezi hili lililochukua takribani siku tano.

Kundi la kwanza lilipanda Mlima Kilimanjaro kwa utaratibu wa kawaida hadi kilele cha Uhuru na kushuka chini kwa kukimbia na kufika katika eneo la Kreta walilolitumia kucheza michezo mbalimbali ya kuruka vikwazo.

Aidha, kundi la pili nalo lilipanda kwa utaratibu wa kawaida, na baada ya kufika kilele cha Uhuru walishuka chini hadi katika Lango la Mweka kwa kukimbia.

Michezo hii ambayo imefanyika kwa mara ya kwanza kwenye Mlima Kilimanjaro inafahamika duniani kama Altitude Obstacle Course Races World Championships, ililenga kuunganisha pamoja watalii kutoka mataifa mbalimbali duniani kushiriki utalii wa michezo kwa pamoja ambayo pia ni mojawapo ya bidhaa za utalii zinazopatikana katika Hifadhi ya Kilimanjaro.

Waanzilishi wa michezo hiyo David Pickles na Rob Edmond wamesema michezo ya mwaka huu imefanikiwa sana kwa kuwa Mlima Kilimanjaro unazo sifa zote za kimsingi za kuwezesha kutimia kwa malengo ya michezo hii. Wameamua kuwa litakuwa ni tukio la kila kwaka kwa Mlima Kilimanjaro ambapo watu kutoka mataifa yote duniani wataalikwa kushiriki.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad