HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, September 28, 2021

OFISI YA KANDA YA ZIWA YATOA MAFUNZO KWA WACHIMBAJI WADOGO

Kaimu Meneja wa Ofisi ya Kanda ya Ziwa, Danstan Mkapa (kulia, picha ya kwanza) akiwasilisha mada iliyohusu majukumu ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali wakati wa mafunzo kwa wachimbaji wadogo na wafanyabiashara wa kemikali yaliyofanyika katika kijiji cha Ng’wakitolyo mkoani Shinyanga tarehe 23 Septemba, 2021. Mkurugenzi wa Huduma za Udhibiti, Daniel Ndiyo (kulia) akifungua mafunzo ya siku moja kwa wachimbaji wadogo na wafanyabiashara wa kemikali yaliyofanyika katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Ng’wakitolyo iliyopo katika kijiji cha Ng’wakitolyo mkoani Shinyanga tarehe 23 Septemba, 2021.

Akiongea wakati akifungua mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Huduma za Udhibiti, Daniel Ndiyo, alisema mafunzo hayo yametolewa kwa wadau hao kwa malengo makuu matatu ambayo ni kuwapa uelewa wa Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali za Viwandani na Majumbani Namba 3 ya Mwaka 2003 pamoja na Kanuni zake za 2020, kuwapatia uelewa wa wa matumizi salama na madhara ya kemikali na kuwapatia uelewa wa umuhimu wa kujisajili na namna ya kujisajili kama wadau wanaotumia kemikali.

Mwezeshaji wa mafunzo kutoka Mamlaka, Tupeligwe Mwaisaka, akiwasilisha mada kuhusu Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali za Viwandani na Majumbani kwa washiriki wa mafunzo yaliyofanyika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Ng’wakitolyo, Shinyanga. CHINI: Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakiongozwa na Afisa Mtendaji wa Kata ya Ng’wakitolyo Samwel Lutonjo (kushoto) wakifuatilia mada ilipokuwa inawasilishwa.




Baadhi ya Washiriki wa mafunzo wakiuliza maswali na ufafanuzi kuhusiana na mada mbalimbali zilizowasilishwa wakati wa mafunzo kwa watumiaji na wafanyabiashara wanaojihusisha na kemikali yaliyofanyika leo katika kijiji cha Ng’wakitolyo mkoani Shinyanga.
Mwezeshaji wa mafunzo kutoka Mamlaka, Ofisi ya Kanda ya Ziwa, Boaz Mizar (kulia), akiwasilisha mada kuhusu Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali za Viwandani na Majumbani kwa washiriki wa mafunzo yaliyofanyika kijiji cha Ng’wakitolyo, Shinyanga leo.



  Mkurugenzi wa Huduma za Udhibiti, Daniel Ndiyo (aliyekaa katikati) akiwa pamoja na Kaimu Meneja wa Ofisi ya Kanda ya Ziwa, Danstan Mkapa (aliyekaa kushoto), Afisa Mtendaji wa Kata ya Ng’wakitolyo, Samwel Lutonjo (wa pili kulia), Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Ng’wakitolyo, Glory Urio (aliyekaa kulia) wakiwa pamoja na washiriki wengine wa mafunzo mara baada ya kukamilika mafunzo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad