HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, September 20, 2021

OFISA HABARI KLABU YA GOFU LUGALO, ASKARI WALIOBUKA NA USHINDI MICHUANO YA MAJESHI WAPONGEZWA

Na Mwandishi Wetu

OFISA  Habari wa Klabu ya Gofu ya. Lugalo Kapteni Selemani Semunyu na askari walioibuka na Ushindi katika Mashindano ya  Kombe la Mkuu wa Majeshi wapongezwa kwa Mafanikio na Kulitangaza Vyema Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania katika Michezo.

Pongezi hizo zimetolewa na Mnadhimu Mkuu  wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Luteni Jenerali Mathew Mkingule wakati wa hafla ya ufungaji Mashindano ya Kombe la Mkuu wa Majeshi kwa Mchezo wa Golf.

" Nimpongezea Kapteni Semunyu kama hamjui umahiri wake ulianza kuonekana akiendesha kipindi Cha Dk 45 ITV na Sasa tunajivunia kuwa na mtu wa aina yake." amesema Luteni Jenerali Mkingule.

Amesema wanatambua uwezo wake ndio maana Jeshi likaona umujimu kuwa nae na Umahiri huo wamekuwa wanauona katika majukumu yake katika kuitangaza JWTZ na nchi kwa Ujumla  kupitia Vyombo vya Habari.

Amengeza kutokana na Umahiri wake na jitihada za kulitangaza jeshi na nchi hasa katika Michezo atafikisha kwa Mkuu wa Majeshi taarifa ya  kazi Nzuri inayofanywa sambamba na Wachezaji wa Gofu Askari walioshinda Mashindano haya.

Aidha  amewapongeza Askari wa Klabu ya Golf ya Lugalo walioshinda katika mashindano hayo kwani alisema  imedhihirisha namna walivyojituma na hatimaye kushinda.

"Askari mlioshinda mmefanya kazi kubwa ya kuletea sifa JWTZ na Taifa kwa Ujumla hakuna budi kupongezwa sambamba na Mwenyekiti kwa kuwalea vizuri kimchezo mpaka kufikia hapo" Alisema Luteni Jenerali Mkingule.

Pia alisema JWTZ ipo katika mpango wa kuhakikisha inajenga Viwanja vya Golf katika Mikoa Mwingine Kama vile Arusha na Iringa eneo la Mafinga.

Awali akimkaribisha Mgeni rasmi Mwenyekiti wa Klabu ya Golf ya Lugalo Brigedia Jenerali Mstaafu Michael Luwongo aliomba Jeshi kukamilisha ahadi ya Ujenzi wa Uwanja Jijini Dodoma.

Aidha alisema Kama Klabu imejiandaa kutengeneza wataalam watakaofundiaha mchezo huo mahala popote itakapo hitajika.

Mshindi wa Jumla wa Mashindano hayo Ni Mchezaji Victor  Joseph kutoka Klabu ya Dar ES Salaam Gymkhana.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad