Naibu waziri wizara ya Viwanda na Biashara awahakikishia wawekezaji nchini utatuzi wa changamoto zinazowakabili - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, September 21, 2021

Naibu waziri wizara ya Viwanda na Biashara awahakikishia wawekezaji nchini utatuzi wa changamoto zinazowakabili

 

NAIBU Waziri Wizara ya Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe (Mb) Leo tarehe 20 Septemba, 2021 amefanya ziara katika Viwanda Vinne vilivyopo eneo la Viwanda la TAMCO Kibaha na Chalinze Mkoani Pwani.

Mhe. Kigahe amesema kuwa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan imedhamiria kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara na kutatua changamoto za wawekezaji.

Mhe. Kigahe ameyasema hayo alipotembelea kiwanda cha kuua mazalia ya mbu kinachoitwa Tanzania Biotech Products Ltd (TPBL). 

Kiwanda hiki kinazalisha dawa za kuua mazalia ya mbu na sasa kipo katika Mpango wa kuanza kuzalisha dawa za mimea.

Kaimu Mkurugenzi Mwendeshaji wa shirika la maendeleo la Taifa (NDC) Bi. Rhobi Sattima amesema kuwa menejimenti ya kiwanda imejipanga kuingia katika masoko ya SADC, AfCTA na masoko mengine ili kutanua wigo wa masoko wa bidhaa hii na nchi mbalimbali zimeshaanza kununua zikiwemo Eswatin, Comoro, Botswana, Kenya, Angola na pia wamekuwa na wateja wa ndani ya nchi kama Ifakara Institute, Zanzibar.

Aidha, Mhe. Kigahe ametembelea kiwanda cha Hester Biosciences Africa Limited kilichopo eneo la TAMCO Kibaha kinachozalisha aina 37 za chanjo za wanyama na ndege, ambazo ni kinga kwa kwa magonjwa 16 ya ng’ombe, kuku, mbuzi, kondoo, punda, farasi na baadae chanjo ya nguruwe.

Naye Mkurugenzi wa kiwanda cha Hester Biosciences Africa Limited Dkt. Furaha Mramba amesema kuwa uwekezaji wa kiwanda  kinategemea kuajiri wafanyakazi wa kudumu 200 na ajira zisizo za kudumu zipatazo 100 na mpaka sasa kiwanda kina waajiriwa wa kudumu 33 ambao wamepatiwa mafunzo mbalimbali ndani na nje ya nchi.

Ameongeza kwa kusema kuwa chanjo ya kwanza itaingia sokoni mwanzoni mwa mwezi Oktoba 2021, Aidha Dkt. Mramba ameeleza changamoto za kiwanda ikiwa ni Barabara pamoja na Umeme wa kukatika mara kwa mara unaopelekea kuharibika kwa mashine.

Mhe. Kigahe ametembelea pia kiwanda cha kutengeza vifungashio cha Global Packaging Limited kilichopo eneo la TAMCO Kibaha pamoja na kiwanda cha kuunganisha magari cha GF Trucks kilichopo katika eneo la TAMCO Kibaha na kujionea vipuri vya magari vinavyounganishwa kiwandani hapo.

Mhe. Kigahe amehitimisha ziara yake kwa kutembelea kiwanda cha kutengeneza malumalu cha KEDA kilichopo Chalinze Mkoani Pwani, kiwanda hiki chenye eneo lenye ukubwa wa heka 140, uwekezaji wake ni Dora za kimarekani milioni 70 na kimeajiri wafanyakazi wa kudumu 1,000 na wasio wa kudumu ni zaidi 3,000.

“Jukumu la Serikali ni kuweka miundo mbinu wezeshi kwa ajili ya wawekezaji wote nchini ambapo sekta binafsi ndio mhimili wa ufanyaji biashara, lakini Viwanda hivi vimetoa fursa kwa watanzania wengi kwani viwanda hivi kwa asilimia kubwa vinatoa malighafi zake ndani ya nchi hivyo vimetengeneza ajira kwa watanzania lakini pia vinaongeza pato la taifa.Hivyo nawaomba wawekezaji wawe na Imani na serikali yetu na tutawalinda wawekezaji kwa nguvu zote” Amsema Mhe. Kigahe.
No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad