Mtango kuzichapa na Mmalawi usiku wa Swahiliflix Rising Star Oktoba 13 - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, September 22, 2021

Mtango kuzichapa na Mmalawi usiku wa Swahiliflix Rising Star Oktoba 13

 


Na Mwandishi wetu

Dar es Salaam. Bondia nyota nchini Salimu Jengo atapanda ulingoni Oktoba 13 kuwania mkanda wa Shirikisho la ngumi za kulipwa Afrika (ABU) dhidi ya bondia Hannock Phiri kutoka Malawi.

Pambano hilo la raundi 12 la uzito wa Super Light  limeandaliwa na kampuni za Swahiliflix  na Win Win Sports Promotion  la uzito wa super light la raundi 12 litafanyika kwenye ukumbi wa Mtana uliopo kwenye jengo la  Millenium Tower 2, Makumbusho, jijini.

Mkurugenzi wa masoko wa Swahiliflix  Amos Chibaya alisema kuwa mkanda huo upo wazi na kuamua kumpa nafasi Jengo kuwania mkanda.

Chibaya alisema kuwa pambano hilo litaonyeshwa ‘live’ na mtandao wao wa Swahiliflix  app  ambayo inapatikana Google Play Store na vile vile kupitia Apple TV.

Alisema kuwa mbali ya pambano hilo, pia kutakuwa na ‘vita’ ya pambano la marudiano kati ya bondia Shawn Miller kutoka Marekani na Shaaban Jongo la uzito wa cruiser la raundi nane.

Alifafanua kuwa Miller ameomba kurudiana na Jongo baada ya kupoteza kwa TKO.

“Swahiliflix inayofuraha kuingia katika ngumi za kulipwa nchini kwa kushirikiana na wadau wengine kama Win Win Sports Promotion,  Urban soul, Global Boxing Stars na Onomo hotel. Tunatarajia kuona mapambano makali nay a kusisimua kwani kila bondia amepania kushinda,” alisema Chibaya.

Alisema kuwa mbali ya kuandaa mapambano, kampuni yao pia itasaidia kutoa ushauri ili kuendeleza vipaji vya ngumi za kulipwa kimataifa.

Alifafanua kuwa wamepania kufanya mambo makubwa katika ngumi za kulipwa hapa nchini kupitia mtandao wao wa kimataifa wa Swahiliflix.

Mbali ya mapambano hayo mawili, pia kutakuwa na pambano kali kati ya bondia kutoka Kenya   Ryton Okwiri ambaye atapambana na bondia wa Uganda John Serunjogi ambapo bondia Joseph Sinkala atazichapa na Hamis Maya na Alex Kachelewa atapimana ubavu na Shadrack Ignas.

Pia kutakuwa na pambano la bondia nyota wa Congo Brazaville Adi Ndembo dhidi ya bondia ambaye atatangazwa hapo baadaye.

Kwa upande wake, Jengo alisema kuwa amejiandaa vyema kupambana na Phiri ambaye  alikuja hapa nchini na kumchapa bondia Hannock Phiri kutwaa ubingwa wa WBF Afrika.


Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya Swahiliflix Amos Chibaya (Katikati) akiwatambulisha mabondia, Salim Jengo (kulia) and Hamis Maya ambao watapambana na wapinzani wao Oktoba 13 kwenye ukumbi wa Mtana wa  Millenium Tower, Makumbusho.

Bondia Salim Jengo (kushoto) akizungumza
Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya Swahiliflix Amos Chibaya  (Katikati) akielezea pambano hilo. Kushoto ni bondia Salim Jengo na kulia ni katibu mkuu wa kamisheni ya ngumi za kulipwa nchini, Yahya Poli.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad