MSANII KIZAZI KIPYA ATAMANI KUFANYA KAZI NA SAUTI SOL - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, September 27, 2021

MSANII KIZAZI KIPYA ATAMANI KUFANYA KAZI NA SAUTI SOL

MSANII chipukizi katika fani ya Muziki, Mavazi na Filamu, Regina Beraldo Kihwele maarufu Gynah anatamani kufanya kazi na bendi ya muziki ya Sauti Sol. Lakini kwenye nyimbo zake alizozitumbuiza wakati wa usiku wa KAHAWA amemshirikisha Junior.

Ghynah ameyasema hayo mwishoni mwa wiki baada ya kukamilisha uzinduzi wa USIKU WA KAHAWA (COFFEE NIGHT) ambapo alitambulisha kazi zake za Sanaa kwa kuonesha mavazi mbalimbali huku akiimba na kutumbuiza jukwaani nyimbo kadhaa zilizomo kwenye EP yake.Uzinduzi huo umefanyika katika Ukumbi wa Little Theatre jijini Dar Es Salaam.

Gynah amesema kuwa mashabiki wa kazi zake watarajie kupata burudani nzuri kwa kusikiliza nyimbo zake ambazo zitakuwa zimewekwa kwenye Extended playlist (EP) ambapo ametumbuiza nyimbo tano na lakini akiweka kwenye EP nyimbo nane mashabiki watapata burudani Zaidi.

Aidha, Regina (Gynah) ambaye amesajiliwa na BASATA, ameteuliwa kuwania Tuzo ya Msanii Bora wa Kike (Best female Actress) kupitia LIPFF FESTIVAL 2021 Afrika ambapo Tuzo hizo zitafanyika mwishoni mwa mwaka huu 2021 nchini Kenya.

Tuzo hizi zinashindaniwa na Wasanii wengine kutoka Afrika ya Kusini, Kenya Cameroon, Uganda, Tanzania na Morocco.

Hivi karibuni Regina (Gynah) ameshiriki pia katika Filamu ijulikanayo "Mulasi" chini ya Muongozaji na Mtayarishaji wa Filamu mahiri kutoka Riccobs Ent. Honeymoon Aljabri, Mtanzania anayeishi nchini Marekani.

Hata hivyo Gynah amesema kuwa wasanii wengine wafanye kazi zao kwa bidii kwani kazi ya mziki ni ngumu. Licha ya hilo amewaomba mashabiki wake kukaa mkao wa kula kwani mwakani 2022 anakamakubwa ya kuwashirikisha.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), Dkt. Kiagho Kilonzo amesema kuwa Baraza la Sanaa Tanzania wanamtia moyo Gynahy kwa kazi anazozifanya kwani anaimba, anaigiza na ni mwanamitindo hivyo serikali ipo kwanajili yao.

Hata hivyo Dkt. Kilonzo amewaasa wanasanii chipukizi kutembelea Baraza la Sanaa Tanzania ili kujisajili bila kufanya hivyo wanakuwa wanapoteza haki zao za msingi.

Afisa Sanaa kutoka Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), Ibrahim Ibengwe amesema kuwa kama mdau wa Sanaa hapa nchini ameguswa na Ghynah anadhihirisha nia yake ya dhati kuhakikisha kwamba anakuwa sehemu ya wadau wa Sanaa hapa nchini.

“Gynahy ni msanii ambaye anajipambanua inaonesha kwamba atafika mbali katika tasinia hii ya Sanaa kwa maana kwamba yeye anavipaji vingi kwani anaimba, ni mwanamitindo na mwigizaji.” Amesema Ibengwe.
Msanii chipukizi katika fani ya Muziki, Mavazi na Filamu, Regina Beraldo Kihwele maarufu Gynah akitumbuiza katika uzinduzi wa usiku wa kahawa uliofanyika katika ukumbi wa Little Theatre jijini Dar Es Salaam.

Msanii chipukizi katika fani ya Muziki, Mavazi na Filamu, Regina Beraldo Kihwele maarufu Gynah akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuzindua EP yake katika Ukumbi wa Little Theatre jijini Dar Es Salaam.
Baadhi ya wadau wa Sanaa wakiangalia Gynah akitumbuiza katika ukumbi wa Little Theatre jijini Dar Es Salaam.Honeymoon Aljabri akizungumza wakati wa uzinduzi wa usiku wa kahawa uliofanyika katika ukumbi Little Theatre jijini Dar Es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad