DKT. GWAJIMA AFUNGUA KONGAMANO LA WAUGUZI KUTOKA NCHI 16 ZA AFRIKA MASHARIKI, KATI NA KUSINI ( ECSACON). - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, September 10, 2021

DKT. GWAJIMA AFUNGUA KONGAMANO LA WAUGUZI KUTOKA NCHI 16 ZA AFRIKA MASHARIKI, KATI NA KUSINI ( ECSACON).

 

Waziri wa Afya Maendeleo ya ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Ngwajima akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuzindua Kongamano la wauguzi kutoa nchi 16 kongamano linalofanyika jijini Arusha.
Mratibu wa kongamano ambaye pia ni makamu mwenyekiti wa umoja wa wauguzi, Ibrahim Mgoo akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ufunguzi wa kongamano jijini Arusha.

Na Woinde Shizza , ARUSHA
ZAIDI ya wauguzi 300 kutoka nchi 16 za Afrika Mashariki, Kati na Kusini wamekutana Jijini Arusha katika kongamano la kisayansi la kimataifa la 14 la wauguzi (ECSACON) kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali yanayohusu uuguzi na pamoja na kuweka mikakati ya namna bora ya kutokomeza vifo vitokanavyo na uzazi.

Akifungua kongamano hilo Waziri wa Afya Maendeleo ya ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Ngwajima amesema kuwa wauguzi hao wamekutana ili kuangalia maendeleo ya tasnia ya uuguzi na ukunga katika mustakabali wa kisayansi wanachangia vipi kwenye maendeleo ya jamii.

“Kama tunavyojua kwenye sekta ya afya karibu nchi zote wauguzi ni sehemu kubwa ya watoa huduma katika huduma za afya hivyo ni lazima tuaangalie maslahi yao vizuri kwani na wao ni ishara ya mwisho ya upendo ambao mwanadamu anaushuhudia kwani mtu anapoingia kwenye mtandao wa huduma za afya mtu anaye kutana nae mara nyingi ni muuguzi,” amesema Dkt Ngwajima.

Amefafanua kuwa lazima wawaangalie wauguzi kuanzia masilahi yao, maendeleo ya taaluma na ustawi wao kwa ujumla kwani mara nyingi maisha ya wagonjwa katika huduma za Afya yanakaa zaidi na wauguzi ikiwemo ICU ambapo muuguzi anaangaika kusaidiana na kudra za Mungu kuokoa maisha ya mgonjwa huyo.

Ameeleza kuwa kama waziri mwenye dhamana ya Àfya ya Tanzania atakuwa msemaji wa umoja wao katika vikao mbalimbali vya mawaziri wa nchi hizo na kwa upande wa Tanzania atazifanyia kazi changamoto zinazowakabili hasa kuboresha maslahi yao kwani hayatoshi kwa ukubwa wa kazi wanaifanya na huku akitolea mfano wa ukonjwa WA UVIKO-19 ambao wauguzi wamekuwa mstari wa mbele kupambana nao.

Kwa upande wake mratibu wa kongamano hilo ambaye pia ni makamu mwenyekiti wa umoja huo Ibrahim Mgoo amesema kuwa kongamano hilo ni muhimu kwa wauguzi kwani huduma zinatakiwa kutolewa kisayansi ambapo pia kutakuwa na mada mbalimbali zitakazojadiliwa ikiwemo kuona ni namba gani wanaweza kusaidia kuondoa vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua.

“Tunataka tuone ni kwa namna gani tunaweza kupunguza vifo vinavyotokana na uzazi lakini pia kuna wajibu wa wananchi kuzingatia wanayoambiwa na wauguzi wanapoenda kliniki kwani wakiyafuata kwa usahihi vifo hivyo hawezi kutokea "Amesema Mgoo.

Aidha amesema kuwa mada nyingine watakayo jadili ni kuhusiana na ugojwa wa UVIKO-19 kwani kama wauguzi wao ndio wako mstari wa mbele kuangalia wagonjwa hivyo watapeana mbinu mpya za kuwahudumia wagonjwa pamoja na wao kujikinga.

Mkutano huo unafanyika kwa siku tatu Jijini humo ambapo mkutano uliopita ulifanyika mwaka 2018 nchini Kenya ikiwa ni mkutano wa 13.

Waziri wa Afya Maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Dkt Dorothy Ngwajima akiongea na waandishi wa habari baada ya kufungua kongamano la kisayansi la 14 la wauguzi na wakunga kutoka nchi 16 za Afrika Mashariki, Kati na Kusini kongamano linaloendelea mkoani Arusha (picha na Woinde Shizza )

066Mratibu wa kongamano la ECSACON Ibrahim Mgoo ambaye pia ni makamu mwenyekiti wa umoja wa wauguzi na wakunga akiongea na waandishi wa habari baada ya ufunguzi wa kongamano lao linaloendelea mkoani Arusha.
(Picha na Woinde Shizza )

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad