HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, September 14, 2021

Demokrasia Makini Wapongezwa Utekelezaji Maagizo Zoezi la Uhakiki wa Vyama

 

Na Mwandishi Wetu, ORPP  Zanzibar

Uongozi wa Chama cha Demokrasia Makini umepongezwa kwa kuzingatia na kutekeleza maelekezo waliyopewa na Ofisiya Msajili wa Vyama vya Siasa (ORPP) wakati wa zoezi la uhakiki wa vyama linaloendelea.

 

Pongezi hiuzo zimetolewa leo Visiwani Zanzibar na Mkuu wa Kitengo cha Usajili toka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Muhidin Mapeyo wakati wa zoezil aala uhakiki wa vyama vya siasa kwa upande wa Ofisi za Vyama vya Siasa zililopo uapnde wa Zanzibar.

 

Mapeyo alisema kuwa amefurahishwa na namna viongozi wa Cha cha Demokrasia Makini kuchukua hatua za haraka kutekeleza maelekezo ambapo wameyakuta maboresho hayo katika Ofisi za Zanzibar ikiwa ni siku chache tu tangu wapewe maelekezo hayo katika uhakiki ulifanyika katika Ofisi za Makao Makuu ya chama hicho zilizopo jijini Dar es Salaam.

 

"Kipekee kabisa niwapongeze kwa namna mlivyojipange na kuonesha umakini katika kutekeleza yale yote ambaye tumekuwa tukiwaelekeza katika kuboresha uendeshaji wa shughuli za chama chenu" alisema Mapeyo.

 

Alisema kuwa chama hicho kimeonesha kwa vitenda akitolea mfano wa maelekezo waliyotoa wakati wa zoezi hilo jijini Dar es Salaam hivi karibuni, kuwa ni pamoja na chama hicho kuandaa kitabu kwa ajili ya utunzaji wa taarifa za fehda na kuziandaa kwa kuzingatia kanuni za fedha za  Sheria ya Vyama vya siasa jambo ambalo wamekuta limefanyiwa kazi.

 

Katika hatua nyingine Mapeyo ametoa rai kwa vyama vya siasa kuwa na mawasiliano ya viongozi kutoka Ofisi za Makao Makuu na zile ofisi ndogo zilizopo Zanzibar ili kurahisisha ufanisi kama iliyojitokeza kwa Chama cha Demokrasia Makini.

 

Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ikiwa mlezi wa vyama vya siasa inayosimamia Sheria ya Vyama vya Siasa Sura 258 na Sheria ya Gharama za Uchaguzi Sura ya 278 inaendesha zoezi la uhakiki kila mwaka kwa lengo la kufuatila utekelezaji wa sheria hizo ambapo kwa mwaka huu zoezi hilo lilianza tarehe 30 Agosti 2021 jijini Dar es Salaam na kuitimishwa tarehe 10 Septemba 2021 kwa kuhakiki vyama 18 kati ya 19 vyenye usajili wa kudumu, na hatimaye kuhamia katika Ofisi za Vyama hivyo upande wa Zanziba lililoanza jana tarehe 13 Septemba 2021 na linatarajiwa kukamilika tarehe 22 Septemba 2021 kwa upande wa Zanzibar, kabla ya kufikia tamati tarehe 28 Septemba 2021 jijini Dodoma. (Mwisho)

Mkuu wa Kitengo cha Usajili toka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Muhidin Mapeyo akimkabidhi nakala za Sheria zinazosimamiwa na Ofisi ya Msajili pamoja na Kanuni zake Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia Makini, Bw. Amir Hassan Amir wakati wa zoezi la Uhakiki wa Vyama vya siasa katika Afisi Ndogo za Makao Makuu ya chama hicho zilizopo Visiwani Zanzibar leo. Timu kutoka ORPP ipo Visiwani humo kwa ajili ya kutekeleza jukumu la kisheria la kukagua uhai wa vyama lililoanza rasmi tarehe 30 Agosti 2021 jijini Dar es Salaam.
Mkukaguzi wa Ndani wa Hesabu toka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Bw. Peter Lyimo akikagua nyaraka za fedhaza Chama cha Demokrasia Makini wakati wa zoezi la uhakiki wa yyama vya siasa katika Afisi Ndogo za Makao Makuu ya chama hicho zilizopo Visiwani Zanzibar leo. Aliyesimama kushoto ni Katibu Mkuu wa Chama hicho, Bw. Amir Hassan Amir na katika ni Mkuu wa Kitengo cha Usajili toka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Muhidin Mapeyo.
Afisa Sheria toka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Bi. Grace Mushi akifuatilia utekelezaji wa amelekezo ya kurejista ordha ya wanachama kwa njia ya Tehama wakati wa zoezi la uhakiki wa yyama vya siasa katika Afisi Ndogo za Makao Makuu ya Chama ca Demokrasia Makini zilizopo Visiwani Zanzibar leo. Aliyekaa ni Katibu Mkuu wa Chama hicho, Bw. Amir Hassan Amir.
Baadhi ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Demokrasia Makini wakifuatilia zoezi la uhakiki lililokuwa linaendeshwa na timu kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa (ORPP) Makao Makuu leo katika Afisi Ndogo za chama hicho zilizopo Visiwani Zanzibar.

Afisa Mkaguzi wa Ndani toka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Bw. Mussa Boma (kushoto) akifuatila maelezo kutoka kwa viongozi wa Chama cha Demokrasia Makini wakati wa zoezi la uhakiki wa yyama vya siasa katika Afisi Ndogo za Makao Makuu ya chama hicho zilizopo Visiwani Zanzibar leo. Wengine ni baadhi ya viongozi wa chama hicho upande wa Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad