HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, September 2, 2021

DC IRINGA :WAZAZI WATAKAOWAOZESHA WATOTO KUKIONA CHA MTEMA KUNI

 Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akigua mmoja ya shule za msingi zilizopo katika tarafa ya kiponzero ambapo kuna wanafunzi wa darasa la saba wanatarajia kuhitimu elimu ya msingi hivi karibuni

Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akigua mmoja ya shule za msingi zilizopo katika tarafa ya kiponzero ambapo kuna wanafunzi wa darasa la saba wanatarajia kuhitimu elimu ya msingi hivi karibuni

Na Fredy Mgunda,Iringa.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa ameonya kuwatia mbaroni na kuwafikisha Mahakamani wazazi watakaobainika kuwashawishi watoto Wao kufeli kwa makusudi mitihani ya kuhitimu darasa la Saba kwa lengo la kuwaozesha na ama kwenda kuwatumikisha katika kazi za ndani nje ya Wilaya hiyo.

Akizungumza Kwenye ziara ya kusikiliza kero za Wananchi mkuu wa Wilaya hiyo Mohamed Hassan Moyo alisema kuwa kumekuwa na tabia ya Wananchi kukatisha ndoto za watoto kwa kuwashinikiza watoto wa kike kuolewa badala ya kuendelea na masomo kutokana na tamaa ya fedha inayowakabili.

Moyo alisema kuwa wilaya ya Iringa imekuwa moja ya wilaya zinazoongoza kwa ukatili wa kijinsia hasa dhidi ya watoto wa kike akiwataja wazazi ama walezi kuwa sehemu watu wanaochochea kuongezeka kwa ukatili huo wakishitikiana na baadhi ya viongozi wa vijijini kwa kuendelea kuficha uhalifu wanaotendewa watoto hao wa kike.

Akiwa katika Ziara yake tarafa ya Kiponzero Mkuu wa Wilaya amewaagiza viongozi wa vijiji na kata Wilayani humo kufanya sensa ya watoto watakaoanza mitihani ya kuhitimu darasa la Saba mwaka huu na kufuatilia mwendo wao Kabla na baada ya kuhitimu lengo likiwa ni kupata Taarifa sahihi zinazowahusu Ili kuwalinda wasiozeshwe ama kurubuniwa kwenda kufanya kazi za ndani katika maeneo mbalimbali ya Miji.

Moyo alisema kuwa watoto wa kike wanahaki ya kusoma na kuzifikia ndoto zao kama ilivyokuwa kwa wanawake wengine wenye mafanikio makubwa dunia kwa kuwa walifanikiwa kuiishi ndoto yao kutokana na wazazi kuwakuza kwenye malezi bora.

Wakiongea kwenye mikutano ya hadhara inayongozwa na mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo wananchi hao walisema kuwa kumekuwa na tabia ya wazazi kuwakatisha masomo kwa makusudi watoto wao kwa tama ya fedha kidogo ambazo zimekuwa zikiua ndoto za watoto hao.

Walisema kuwa wameyasikia maagizo ya mkuu wa wilaya hivyo watahakikisha wanafanya ulinzi shirikishi kwenye vijiji vyao ili kuhakikisha kuwa wanakuwa na watoto ambao watakuwa huku wakiishi kwa lengo la kutimiza malengo yao.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad