HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, August 1, 2021

Waziri Dk.Ndugulile azindua mfumo wa Uombaji wa Leseni kwa njia ya Mtandao

 *Aipongeza TCRA kwa jitihada za katika uboreshaji wa huduma


*Bashungwa asema mabadiliko makubwa yatokea katika uanzishaji wa Televisheni na Radio

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
Serikali imesema kuwa sekta ya mawasiliano inakua kwa kasi katika uwekezaji nchini hivyo ukuaji huo usiwe na vikwazo ndio umeanzishwa Mfumo wa uombaji leseni kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuharakisha Uchakataji wa leseni kwenda haraka tofauti na mfumo wa zamani wa makaratasi.

Hayo ameyasema Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dk.Faustine Ndugulile wakati uzinduzi wa Mfumo wa Uombaji leseni katika Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA uliofanyika jana jijini Dar es Salaam.

Dk. Ndugulile amesema mfumo huo utasaidia uwajibikaji na uwazi pamoja na kupunguza muda wa ucheleweshawaji wa leseni kwa waombaji.

Waziri huyo amewaagiza TCRA kumalizia mchakato wa mapitio ya tozo mpya za maudhui ya mtandaoni hadi kufikia Septemba Mosi mwaka huu ziwe zimefanyiwa kazi ili aweze kuwasilisha kwa Rais Samia Suluhu Hassan na kuongeza kuwa serikali imejipanga kuboresha sekta ya mwasiliano nchini ambapo mfumo wa uombaji leseni ndogo kwa sasa ni siku tatu hadi tano huku leseni kubwa ni siku 45 kutoka mwaka mmoja ilivyokuwa hapo awali.

"Sasaivi dunia inafanya mabadiliko makubwa katika sekta ya mawasiliano na serikali imejipanga kufanya mabadiliko hayo, ili kuhakikisha wawekezaji hawapati changamoto tulikuwa na changamoto ya ucheleweshaji wa huduma ya utolewaji leseni kwa wawekezaji wanaohitaji kwenda kwa haraka zaidi "ameema.

Pia Ndugulile aliwapongeza TCRA kwa kuwa wazalendo kwa kutumia wataalamu wa ndani katika kutengeneza mfumo huo na ndicho kuwa kitu kizuri kuliko ukitengenezwa na watu wa nje ya nchi.

Aidha Dk Ndugulile alitoa wito kwa wananchi kujitokeza kuwekeza katika kuomba leseni za usikivu wa vituo vya redio katika Wilaya 69 nchini ambapo matangazo ya maombi yatafanyika hapo baadae

"Tunataka kufanya uhamasushaji wa wawekezaji katika usikivu wa redio katika Wilaya 69 watanzania wajitokeze kwani baadhi ya maeneo hakuna usikivu wa redio"alisema.Naye Waziri wa Habari,Utamduni ,Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa,amesema mfumo huo utaleta weledi na ufanisi katika vyombo vya redio na televisheni .

Pia Bashungwa, alisema mfumo huo utasaidia kuondoa vitendo vya rushwa kwa watoa huduma na kuleta mageuzi makubwa katika sekta ya Habari.Aidha aliongeza kuwa serikali haiitamfumbia macho mtumishi yeyote atakaye sababisha ucheleweshaji katika kutoa huduma hiyo kupitia Mfumo kwani anaonekana katika mfumo.

"Mtumishi yeyote ambaye atalega lega na kusababisha kuchelewesha serikali haiitamfumbia macho,na mfumo huu utaongeza weledi na ufanisi na katika vyombo vyetu vya habari "alisema.Naye Mkurugenzi wa Leseni na Udhibiti kutoka (TCRA )John Daffa,amesema mfumo huo utasaidia maombi ya leseni hizo kufanyiwa tasmini na wataalamu kwa muda mfupi tofauti na hapo awali.

Pia alisema mfumo huo utasaidia kupunguza muda wa uchakataji maombi ya leseni kutoka mwaka mmoja hadi siku tatu hadi tano kwa leseni ndogo.
Waziri wa Habari, Utamduni,Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa akizungumza kuhusiana na mapinduzi ya Sekta ya Utangazaji pamoja na Mfumo wa Uombaji leseni kwa njia ya Mtandao utapolea mapinduzi makubwa nchini.

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dk.Faustine Ndugulile akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mfumo wa utoaji wa leseni kwa njia ya Mtandao wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) uliofanyika jijini Dar es Salaam.


Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dk.Faustine Ndugulile pamoja na Waziri wa Habari, Utamduni,Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa wakiwa katika uzinduzi wa Mfumo wa Uombaji leseni kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dk.Faustine Ndugulile pamoja na Waziri wa Habari, Utamduni,Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa wakiwa katika uzinduzi wa Mfumo wa Uombaji leseni kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) uliofanyika jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad