Na. Abel Paul Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Arusha ACP-JUSTINE MASEJO leo tarehe 18.08.2021ametoa
taarifa kwa vyombo vya habari na amesema kuwa tarehe 17.08.2021 muda
wa 09:00 Alasiri katika ofisi ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco)
Mkoa wa Arusha zilizopo katika mtaa wa Old line kata ya Themi
halmashauri ya Jiji la Arusha, Jeshi la Polisi Mkoani hapa lilifanikiwa
kuwakamata watu watatu ambao ni GIDIONI WILLIAM miaka 26 mkazi wa
Sombetini, RICHARD FRANK miaka 20 Mkazi wa Daraja la II, GODSON ERICK
miaka 20 Mkazi wa Moshono wakijifanya watumishi wa Shirika la Umeme
(Tanesco) Mkoa wa Arusha.
ACP- MASEJO amesemakuwa Watuhumiwa hao
walikamatwa mara baada ya kupokea taarifa toka kwa raia wema kwamba,
wamekuwa wakijihusishsa na wakuwadanganya wananchi ambao wanahitaji
huduma za kuunganishiwa umeme kuwa wao ni Maofisa wa Shirika hilo na
wana uwezo wa kuwapatia huduma wanazozihitaji kwa njia ya mkato, ndipo
timu ya makachero wa Polisi wakirikiana na maofisa wa shirika la umeme
waliweka mtego na kufanikisha kuwakamata watuhumiwa hao.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Arusha amesema kuwa Kutokana na tuhuma hizo Jeshi la
Polisi Mkoani hapa tunaendelea kuwahoji watuhumiwa ili kupata mtandao
mzima unaohusika na vitendo hivyo vya kitapeli katika ofisi za shirika
la umeme (Tanesco) Mkoa wa Arusha.
Ameendelea kusema kuwa pindi
upelelezi utakapokamilika jalada litapelekwa ofisi ya Taifa ya Mashtaka
kwa hatua zaidi za kisheria.
Kamanda Masejo ametoa wito kwa
wananchi kuzitumia ofisi na taasisi za umma ambazo zipo kwa ajili yao
pindi wanapohitaji huduma yoyote hali hii itasadia kuwakwepa walaghai
ambapo wanaweza kuwaingiza katika matatizo au hasara. Aidha naendelea
kuwaomba wananchi wa mkoa wa Arusha kuendelea kushirikiana na Jeshi la
Polisi Mkoa wa Arusha.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha ACP-JUSTINE MASEJO
No comments:
Post a Comment