HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, August 23, 2021

VODACOM TANZANIA FOUNDATION YATAMBULIWA KWA KUBORESHA ELIMU KUPITIA TEKNOLOJIA

 

Mamlaka ya Elimu ya Tanzania (TEA) imetoa cheti cha kutambua mchango enedelevu wa Vodacom Tanzania Foundation (VTF) kwa ukuaji wa sekta ya elimu nchini. Kutambuliwa huku kunatokana na dhamira ya kampuni kutumia mtandao wake mpana kutimiza ahadi yake ya kutomuacha mtu yoyote nyuma kwa kuenga ushirikishwaji katika elimu kupitia teknolojia.

Elimu jumuishi ni moja ya misingi mikuu ya kampuni ambapo kupitia mipango inayoendeshwa kwa teknolojia, VTF inalenga kuleta usawa katika upatikanaji wa elimu bora kwa wanafunzi na kuwapatia waalimu vifaa stahiki kwa kujenga upokeaji wa madarsa mtandaoni nchini. Foundation inafanya kazi kwa kushirikiana na serikali kupita Wizara ya Elimu kusaidia kufikiwa malengo ya kielimu ya taifa na kuendeleza kasi ya ufikiaji wa Lengo Endelevu(SDG) namba 4 linalolenga elimu bora ambapo, hadi sasa, Zaidi ya wanafunzi 100,000 wametumia jukwaa lisilo na gharama kupitia mradi wa Vodacom Tanzania Foundation uitwao E-Fahamu (awali ukijulikana kwa jina la Instant School).

Uwekezaji wa VTF kwenye elimu unatumia upana na ubora wa mtandao wa Vodacom unaolenga kujenga elimu bora na jumuishi nchini Tanzania ikiwa ni sehemu ya mpango wa Foundation iliobebwa na kauli mbiu “Connecting for Good” inayohakikisha hakuna mtoto anayeachwa nyuma. Kupitia uwekezaji wake endelevu kwenye sekta hii, Foundation inasaidia lengo kuu la TEA kuleta elimu bora na sawa kwa wote. TEA ilianzishwa mwaka 2001 kusimamia Mfuko wa Elimu ulioanzishwa kwa lengo la kusaidia jitihada za serikali kwa kufadhili maendeleo ya elimu ya ngazi zote Tanzania bara na elimu ya juu Tanzania visiwani.

Mradi wa E-Fahamu unaonyesha uwezo mkubwa wa mtandao wa Vodacom na teknolojia kwa pamoja kujenga uchumi stahimivu kupitia uwekezaji makini ambapo tovuti zote zenye maudhui ya elimu hayatozwi kwa watumiaji ili kuwawezesha kufikia shule na vyuo bila gharama. “Tunajivunia kupokea heshima kubwa kama hii kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Heshima hii inaongeza azma yetu kuendelea kushirikiana na serikali kuleta elimu bure kwa wote.” Alisema Rosalynn Mworia, Mkurugenzi wa Foundation.

E-Fahanu ni jukwaa linalowapatia waalimu vifaa vinavyoboresha utoaji wa masomo na kuwapa wanafnzi maudhui mengi kuwawezesha kujifunza kwa kasi yao wenyewe na kuelewa vizuri zaidi yanayofundishwa darasani. Imejaza pengo linalotokana na upungufu wa vitabu kwa kutoa maudhui mengi kutosha bila gharama. Mradi unawasaidia waalimu kuwa na wakati rahisi Zaidi kupanga masomo yao kutokana na upatikanaji kwa haraka maelezo wanayohitaji. Mmoja wa waalimu hao ni Mwalimu Damian Mtono wa Shule ya Sekondari ya Mtakuja. “Nilikuwa napitia vitabu kuandaa notes kwa wanafunzi wangu, inachukuwa muda na juhudi nyingi na wengi wetu tumekuwa tukipata wakati mgumu kwa sababu kwanza inabidi kuvipata vitabu vyenyewe ambavyo viko vichache,” alisema Mwalimu Damian.

 “Instant Schools ilibadilisha kila kitu. Niliweza kupata maudhui kwa haraka na urahisi Zaidi kutokana na kutumia mpango huu nimekuwa mwalimu bora wa Bilojia wilayani wanafunzi wangu asili mia 71 wakipasi,” aliongezea.

Masomo ya sayansi kwa jumla yanaonekana kuwa magumu kuelewa lakini masomo yaliyko kwenye jukwaa la Instant Schools ni rahisi kusoma na kuelewa na yanaelezea kwa upana somo lote. Wanafunzi pia wanasifu faida za jukwaa. “Jukwaa la Instant Schools ni zuri kiasi kwamba natumia kuwafundisha wadogo zangu walioko madarasa ya msingi kwa sababu kuna vitabu na maudhui ya shule kuanzia chekechea hadi sekondari.” Alisema Happoiness Juma, wakai huo akiwa mwanafunzi wa shule ya Mtakuja.

Hadi sasa Zaidi ya shule 190 zinatumia jukwaa la Instant Schools. Mradi hu una mingine inayotekelezwa na VTF inafanikiwa kutokana na mtandao mpana wa Vodacom. Vodacom imedhamiria kusaidia maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa kutumia mtandao wake kupambana na changamaoto za kila siku zinazowakumba watu katika jamii. Hii inaendana na mkataba wa jamii wa kampuni kusaidia vipaumbele vya serikali. “Vodacom Tanzania ina minara Zaidi ya 2,000 ya 4G inayoleta mtanado wenye kasi Zaidi nchini. Hii pamoja na kuondolewa gharama kwa tovuti ya elimu inachochea kasi ya engo letu kuwafikia wanafunzi milioni moja ifikapo mwaka 2025,” alisema Rosalynn Mworia.

 “Tumeona mabadiliko makubwa, chanya kupitia mradi huu. Huu mradi unaboresha viwango vya elimu wanayopata wanafunzi, mabadiliko yanayoonekana kwenye ufahamu mkubwa wa maswala ya TEHAMA, kuongezeka kwa kujiamini, kufurahia Zaidi mafunzo na kuboreka kwa viwango mashuleni,” aliongeza.

E-Fahamu ni mradi pacha wa Instant Schools ulioanzishwa mwaka 2013 kwa ushirikiano kati ya Vodafone Foundation na UNHCR kuwapa wakimbizi vijana, jamii zinazowapokea na waalimu wao maudhui ya elimu kupitia mtandao. Kila shule inapata vifaa ikiwa ni pamoja na tablet ya mwalimu na kompyuta kwa wanafunzi. Vifaa vinawekewa maudhui ya nchini inayoendana na mitaala ya kitaifa. Zaidi ya kusaidia mafunzo ya msingi darasani, stadi wanazojifunza wanafunzi kupitia mradi huu zinaongeaz uwezo wao kupata ajira na kuwapatia fursa nyingi zaidi maishani.

Baadhi ya watoto walioko kwenye kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu, mkoani Kigoma wakitumia baadhi ya vifaa vya kujisomea vilivyotolewa na kampuni ya Vodacom Tanzania PLC kupitia Taasisi yake ya Vodacom Tanzania Foundation. Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) hivi karibuni ilitoa cheti kwa kampuni ya Vodacom kwa kutambua juhudi endelevu za kuunga mkono sekta ya elimu hapa nchini



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad