HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, August 24, 2021

UNESCO yaendesha mafunzo kukabili maafa

 Na Mwandishi Wetu, Bagamoyo

SHIRIKA la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO)  linaendesha mafunzo ya wiki mbili kwa wataalamu wa mambo ya  maafa juu ya matumizi ya akili bandia (AI) katika kukusanya takwimu na hivyo kuyakabili kwa wakati mwafaka.

Kwa mujibu wa Mratibu wa Mafunzo  hayo, Ofisa Sayansi Asilia wa Unesco, Keven Robert mafunzo hayo ni sehemu ya mradi unaoendeshwa katika nchi tano za Afrika Mashariki za Kenya, Rwanda, Sudan Kusini, Tanzania, na Uganda ya namna ya kukabiliana na maafa yanayosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi.

Alisema, watu 150 nchini wanatarajiwa kufaidika na mafunzo hayo wakiwemo maofisa kutoka Jukwaa la Maafa nchini, Ofisi ya Waziri Mkuu ambayo ndio huratibu masuala ya maafa na asasi mbalimbali za kiraia na vyuo vya elimu ya juu.

Robert alisema kwamba, kuendeshwa kwa mafunzo kumelenga kuleta teknolojia mpya ya kisasa ya kukabiliana na majanga ikiwa ni pamoja na matumizi ya Tehama katika kurekodi taarifa za asili na za sasa za maafa yanayosababishwa na majanga na maeneo ambayo yana majanga au yako katika hatari ya kuwa nayo.

Mafunzo hayo ni sehemu ya mradi unaotekelezwa na Unesco kwa kushirikiana na  Nchi wanachama kwa ufadhili wa Serikali ya Japan.

Mradi huo wenye sehemu tatu yakiwemo mafunzo pia umelenga kuwezesha nchi zisizokuwa na sera na sheria kuwa na sera na sheria zinazohusu majanga na pia kutoa nafasi kwa waliokuwa nazo kuzirejea kwa lengo la kuingiza maarifa ya kisasa katika ukusanyaji wa takwimu na kukabili majanga.

Alisema, kwa sasa pamoja na matumizi ya akili bandia, majanga pia takwimu zake  hukusanywa na  mifumo ya tehama pamoja na kutumia ndege zisizo na rubani kupiga picha zenye maelekezo yaliyokamilika kama eneo la maafa, idadi ya wahusika na athari zake.

Robert alisema kutokana na ukweli kuwa asilimia 70 ya majanga yanayotokea yanatokana na mabadiliko ya tabia nchi, mafunzo hayo yameunganisha watu wengi zaidi wakiwemo wanaoshughulika na hali ya hewa .

Akizungumzia  kuhusu mafunzo hayo  Ofisa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu kitengo cha maafa, Charles Msangi  alisema yana manufaa makubwa ili kuhakikisha kwamba wadau wote wanajua namna ya kutumia akili bandia katika shughuli za uokozi.

Ofisi ya Waziri Mkuu ndiyo inashughulikia maafa kwa mujibu wa sheria ya Usimamizi wa Maafa namba 7 ya mwaka 2015 na sera ya taifa ya menejimenti ya maafa ya mwaka 2004.

Alisema, ni muhimu kwa wadau wote kuwa na uelewa wa pamoja kuhusu matumizi ya teknolojia ya akili bandia katika ukusanyaji wa takwimu zinazoweza kuchambuliwa hata kubashiri maeneo ambayo yanaweza kupata maafa na kuchukua hatua mapema au kuwa tayari.

“Mafunzo haya ni muhimu kwa sababu Tanzania huwa tunakabiliwa na majanga mbalimbali kama mafuriko na hata ukame  kunakosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi ni muhimu kuwa na elimu juu ya ukusanyaji wa takwimu wa kisasa zaidi” alisema Msangi.

Alisema mafunzo hayo ni sehemu kujiweka sawa kwa wadau kujua kuhusu nyenzo nyingi zinatumika katika kukabiliana na majanga.

Katika miongo kadhaa iliyopita, mabadiliko ya tabia nchi yamesababisha maafa makubwa katika nchi za Afrika Mashariki ambazo zipo katika mradi huo.

Mei 2020, mafuriko yalikumba robo tatu ya taifa la Kenya huku maporomoko ya ardhi yakiripotiwa Bonde la Ufa na kusababisha watu 400,000 kukosa makazi.

Nchini Rwanda mafuriko na maporomoko ya ardhi yalisababisha hasara ya dola za Marekani milioni 225 na nyumba zaidi ya 16,000 ziliharibiwa.


Ofisa Sayansi Asilia na Mratibu wa Mradi wa kukabiliana na maafa kwa nchi za Afrika Mashariki unaotekelezwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa(UNESCO), Keven Robert akizungumza wakati wa mafunzo ya wiki mbili ya wataalamu wa mambo ya maafa juu ya matumizi ya akili bandia (AI) katika kukusanya takwimu na hivyo kuyakabili maafa kwa wakati mwafaka kupitia mradi unaotekelezwa na Unesco kwa kushirikiana na  Nchi wanachama kwa ufadhili wa Serikali ya Japan yanayoendelea Bagamoyo mkoa wa Pwani.
Ofisa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu kitengo cha maafa, Charles Msangi akizungumza wakati wa mafunzo ya wiki mbili ya wataalamu wa mambo ya maafa juu ya matumizi ya akili bandia (AI) katika kukusanya takwimu na hivyo kuyakabili maafa kwa wakati mwafaka kupitia mradi unaotekelezwa na Unesco kwa kushirikiana na  Nchi wanachama kwa ufadhili wa Serikali ya Japan yanayoendelea Bagamoyo mkoa wa Pwani.
Mwakilishi wa Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (NATCOM-UNESCO) Bw. Joel Samwel akitoa salamu za NATCOM wakati wa mafunzo ya wiki mbili ya wataalamu wa mambo ya maafa juu ya matumizi ya akili bandia (AI) katika kukusanya takwimu na hivyo kuyakabili maafa kwa wakati mwafaka kupitia mradi unaotekelezwa na Unesco kwa kushirikiana na Nchi wanachama kwa ufadhili wa Serikali ya Japan yanayoendelea Bagamoyo mkoa wa Pwani.
Ofisa Sayansi Asilia na Mratibu wa Mradi wa kukabiliana na maafa kwa nchi za Afrika Mashariki unaotekelezwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa(UNESCO), Keven Robert akiwasilisha mada katika mafunzo ya wiki mbili ya wataalamu wa mambo ya  maafa juu ya matumizi ya akili bandia (AI) katika kukusanya takwimu na hivyo kuyakabili maafa kwa wakati mwafaka kupitia mradi unaotekelezwa na Unesco kwa kushirikiana na  Nchi wanachama kwa ufadhili wa Serikali ya Japan yanayoendelea Bagamoyo mkoa wa Pwani.
Baadhi ya wataalamu kutoka asasi mbalimbali za kiraia, serikali na vyuo vya elimu ya juu wa mambo ya maafa juu ya matumizi ya akili bandia (AI) katika kukusanya takwimu na hivyo kuyakabili maafa kwa wakati mwafaka kupitia mradi unaotekelezwa na Unesco kwa kushirikiana na Nchi wanachama kwa ufadhili wa Serikali ya Japan yanayoendelea Bagamoyo mkoa wa Pwani.
Picha ya pamoja ya washiriki wanaohudhuria mafunzo ya wiki mbili kutoka asasi mbalimbali za kiraia, serikali na vyuo vya elimu ya juu wa mambo ya maafa juu ya matumizi ya akili bandia (AI) katika kukusanya takwimu na hivyo kuyakabili maafa kwa wakati mwafaka kupitia mradi unaotekelezwa na Unesco kwa kushirikiana na Nchi wanachama kwa ufadhili wa Serikali ya Japan yanayoendelea Bagamoyo mkoa wa Pwani.

 




No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad