RIDHIWANI - WAKAZI WA MJEMBE ,KWAMDUMA KUNUFAIKA NA BWAWA LA MRADI WA MAJI LINALOJENGWA NA RUWASA KWA MIL. 900 - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, August 5, 2021

RIDHIWANI - WAKAZI WA MJEMBE ,KWAMDUMA KUNUFAIKA NA BWAWA LA MRADI WA MAJI LINALOJENGWA NA RUWASA KWA MIL. 900

 


Na Mwamvua Mwinyi,Chalinze

Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete ,ametembelea kuona maendeleo ya Ujenzi wa Mradi wa Bwawa Kubwa la Maji litakalogharimu Shilingi Milioni 900 huko Mjembe, Kwamduma linalojengwa na Wakala wa Maji Vijijini-RUWASA.

Akizungumzia ujenzi huo ,alieleza bwawa hilo ,litakapokamilika litapeleka maji kwa Vitongojj vyote kwa kijiji cha Kwamduma.

Ridhiwani alisema maji safi ni muhimu kwa afya za binadamu hivyo watarajie wakazi hao kuondokana na kero ya maji.

Ridhiwani Pia ameongea na wananchi na kuwaasa kujikinga kupambana na gonjwa la Korona na kwenda kuchanja.

Aliwaondoa hofu na kuwataka wakachanjwe kwa hiari zao na kuwaambia Chanjo hiyo haina madhara .

#AsanteSerikali #KaziInaendelea
 


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad