Rais wa Jamhuri ya
 Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 12 Agosti, 
2021 amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Oman hapa nchini Mhe. 
Balozi  Ali Bin Abdallah Bin Salim Al Mahrouqi aliyemaliza muda wake wa 
uwakilishi hapa nchini, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma. 
Katika 
mazungumzo hayo, Mhe. Balozi Al Mahrouqi amempongeza Mhe. Rais Samia kwa
 utawala wake na kuishukuru Serikali ya Tanzania  kwa ushirikiano mkubwa
 alioupata wakati alipokuwa akitekeleza majukumu yake. 
  Aidha, 
Mhe. Balozi Al Mahrouqi amesema Tanzania na Oman zina uhusiano mzuri na 
wa muda mrefu hivyo kuomba kuendelezwa kwa ajili ya maslahi ya nchi zote
 mbili pamoja na  kuimarishwa biashara. 
Kwa upande wake, Mhe. 
Rais Samia amemhakikishia Balozi Al Mahrouqi kuwa Tanzania itaendeleza 
na kudumisha ushirikiano wake na Oman kwa masalahi ya nchi zote mbili. 
Mhe.
 Rais Samia amemjulisha Balozi huyo kuwa kwa sasa Tanzania inapitia 
sheria na sera zake mbalimbali za biashara ili kujenga mazingira mazuri 
zaidi ya biashara na uwekezaji ikiwa ni pamoja na  kuongeza ufanisi 
katika viwanja vya Ndege na Bandari ili kurahisisha ufanyaji biashara 
baina ya nchi hizi mbili. 
Pia, Mhe. Rais amezitaka Tume za 
pamoja kati ya Tanzania na Oman kukutana na kuzungumza ili kuimarisha 
mambo mbalimbali baina ya nchi hizo. 
Mhe. Rais Samia amemshukuru
 na kumpongeza Mhe. Balozi Al Mahrouqi kwa kazi nzuri ya uwakilishi wake
 hapa nchini katika kipindi cha miaka 4 kwa kudumisha uhusiano kati ya 
Oman na Tanzania. 
  
Jaffar Haniu 
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu.  
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Balozi wa Oman aliyemaliza muda wake hapa nchini Mhe. Ali Bin Abdallah Bin Salim Al Mahrouqi mara baada ya kuwasili Ikulu Chamwino mkoani Dodoma kwa ajili ya kuaga leo tarehe 12 Agosti, 2021. PICHA NA IKULU.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiagana na Balozi wa Oman aliyemaliza muda wake hapa nchini Mhe. Ali Bin Abdallah Bin Salim Al Mahrouqi mara baada ya kuwasili Ikulu Chamwino mkoani Dodoma kwa ajili ya kuaga leo tarehe 12 Agosti, 2021. PICHA NA IKULU.
 

 
 




 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
No comments:
Post a Comment