Mwenge wa Uhuru waanza Mbio zake Mkoani Pwani - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, August 11, 2021

Mwenge wa Uhuru waanza Mbio zake Mkoani Pwani

 

Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhe Abubakar Kunenge leo Agosti 11, 2021 majira ya saa 12 Asubuhi amepokea Mwenge huo kutoka  kwa Mhe.  Martine Shigela Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Kunenge  Ameeleza kuwa Mwenge huo ukiwa Mkoani hapo utakimbizwa katika Wilaya saba za Mkoa huo na kufikia Miradi 87 ambapo Miradi  18 Itafunguliwa Miradi  9 Itawekwa mawe ya Msingi na Miradi 60 Itakaguliwa.

Miradi yote inathamani ya Shilingi  57,311,572,720. Ameeleza Miradi yote imezingatia  Kauli Mbiu ya Mbio Maalumu za Mwenge  wa Uhuru 2021 Isemayo TEHAMA ni Msingi waTaifa  Endelevu  itumie kwa usahihi na Uwajibikaji.

Baada ya kupokea Mwenge huo Mhe Kunenge amekabidhi kwa Mhe Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Zainabu Abdalah.

"Kwa niaba ya Wananchi wa Mkoa wa Pwani, ninayoheshima kubwa kuwakaribisha wakimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa Mkoani Pwani na kwa kipindi chote Mjiskie mpo Nyumbani kwa ndugu zenu wakarimu Wanapwani.

Tayari mwenge wa Uhuru mwaka 2021 umekwishaingia mkoa wa Pwani salama na kupokea na Mkuu wa mkoa wa Pwani Mheshimiwa Abubakhar Kunenge kutoka kwa Mkuu wa mkoa wa Morogoro Mheshimiwa Shigela.
 


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad