HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, August 5, 2021

MURIYA OMAN YAZINDUA MAONESHO YA MAKAZI JIJINI DAR ES SALAAM BAADA YA KUFANYIKA ZANZIBAR KWA MAFANIKIO.

 

 Kampuni ya Muriya ambao wanajishughulisha na mradi mkubwa wa makazi huko Oman, wamemaliza maonyesho yake ya kila mwaka ya makazi huko Zanzibar na wanaendelea na hafla zake za maonesho Dar es Saalam nchini Tanzania

Jijini Dar es Saalam maonyesho ya kuvutia ya makazi yataanza Agosti 4, 2021 katika Hoteli ya Sea Cliff kuanzia saa 4:00 asubuhi hadi saa 1:00 jioni na kuendelea hadi Agosti 6, 2021. Baada ya siku za maonyesho ya makazi Zanzibar, timu ya Muriya ina imani kuwa hafla za Dar Es Saalam zitavutia wageni wengi zaidi watakaovutiwa na kupendekeza kupata fursa za uwekezaji wa mali na makazi huko Oman.

Baada ya kumaliza maonesho yao jijini Dar Es Saalam timu ya Muriya itaendelea na shughuli zao za maonesho nchini Kenya.

Katika siku chache zijazo, timu ya Muriya itaonyesha maendeleo bora ya makazi na fursa za uwekezaji wa kimataifa katika maeneo yake mawili, Jebel Sifah na Hawana Salalah, na kuzindua makazi yake mapya na eneo mpya ya burudani kwa maeneo yote mawili.

Kwa lengo la kuimarisha hadhi ya nchi ya Oman kama eneo muhimu la uwekezaji wa makazi ulimwenguni, hafla za maonesho ya Muriya zitaonesha mtiririko wa hotuba, mawasilisho, mazungumzo ya wataalam, na uchambuzi wa soko la makazi hayo. Kutoka kwenye vyumba hadi majengo marefu ya kifahari (ghorofa) katika jamii zilizoendelea miradi inayotafutwa zaidi ya Muriya kote nchini Oman inaihakikishia mapato bora kuanzia $133,000, hii ni pamoja na makazi ya wanunuzi na familia zao.

Jebel Sifah, mradi wa makazi yaliyoko dakika 40 kutoka mji mkuu wa Muscat yapo eneo lenye  ukubwa wa mita za mraba zaidi ya milioni 6.2.  Ina nyumba za makazi, ambazo ni za kumiliki au kukodisha, sehemu za maegesho ya boti binafsi 84, sehemu za vituo vya kulia na vya kupumzika, pamoja na uwanja wa gofu uliotengezwa na Mhandisi wa viwanja vya gofu maarufu duniani Peter Harradine.

Jebel Sifah, ni eneo lisolokuwa na msongamano wa watu Mjini Muscat, hutoa fursa ya uwekezaji wa aina moja ya kumiliki nyumba katika eneo lililotengenezwa vizuri, pia hukupatia fursa za makazi ya kuvutia zinazokuwezesha kucheza gofu, kufanya utalii wa bahari na kuangalia milima kwa uzuri zaidi.  

Pamoja na eneo la ukubwa wa mita za mraba milioni 13.6, kivutio kikuu cha makazi ya  Muriya Hawana Salalah yaliyopo katika jiji la kitropikana la Salalah katika mkoa wa Kigavana wa Dhofar, Oman. Yalipo makazi hayo ndipo inakopatikana hifadhi ya kwanza ya maji nchini Oman ya Hawana, maegesho ya boti binafsi 170, makazi ya bure na  kumbi za rejareja, migahawa na hoteli. Makazi ya Hawana Salalah hulifanya eneo hili kuwa na nyumba na fursa za uwekezaji.  

Kila mkazi katika eneo la Hawana Salalah hufurahia mandhari nzuri ya bahari, na imejengwa kwa kuzingatia, kuangalia na kuambatana na mitindo anuwai ya maisha, saizi ya chumba kimoja au viwili vya kulala, nyumba za mijini, majengo ya kifahari yaliyotengwa peke yake na majengo ya kifahari yaliyopo pwani ya bahari.

Pamoja na uwekezaji zaidi $ 750 milioni, Muriya wako nyuma ya maendeleo makubwa katika eneo la kiutawala la Sultan wa Oman na wataendelea kuleta maonesho ya makazi ambayo yanawakilisha fursa za kipekee za kuishi na uwekezaji.

Meneja Mradi wa kujenga nyumba za makazi wa Kampuni ya MURIYA, ya nchini Oman, Ghizlane Gouch (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana wakati uzinduzi wa maonyesho ya makazi kwa wakazi Tanzania wanaotka kununua nyumba nchini homu kulia ni Ofisa Mkuu wa Fedha wa kampuni hiyo, Mohamed Abdallah.

Afisa mkuu wa idara ya fedha wa kampuni ya miradi ya ujenzi wa nyumba za makazi ya Muriya nchini Oman, Mohammed Abdallah (kulia), akizungumza na waandishi wa habari, Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa maonesho ya mradi mkubwa wa nyumba za makazi zinazojengwa na kampuni nchini humo. Katikati ni meneja mradi wa kampuni ya Muriya Bi. Ghizlane El Gouch, na mshauri wa miradi hiyo Lubna Al Riyami (kushoto
 Meneja wa mradi wa Kampuni ya ujenzi wa Nyumba za Makazi, nchini Oman, Bi. Ghizlane El Gouch (Left) akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Maonyesho ya mradi mkubwa wa nyumba za Makazi zinazojengwa na kampuni hiyo
Moja ya nyumba zinazojengwa na kampuni ya Muriya ya nchini Oman.

 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad