Kamati Mpya ya Uongozi wa Baraza la Vyama vya Siasa Wakabidhiwa Vitendea Kazi - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, August 27, 2021

Kamati Mpya ya Uongozi wa Baraza la Vyama vya Siasa Wakabidhiwa Vitendea Kazi

 

Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi akimkabidhi vitende kazi Mwenyekiti Mpya wa Baraza la Vyama vya Siasa, Juma Khatibu wakati wa kikao cha kutambulisha Wajumbe wa Kamati ya Uongozi wa Baraza leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza hilo Bibi. Christine Mndeme.

Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Francis Mutungi akisisitiza jambo wakati wa Kikao cha Kamati ya Uongozi ya Baraza la Vyama vya Siasa leo jijini Dar es Salaam. Kikao hicho kimefanyika ikiwa ni mara cha kwanza kwa wajumbe wapya wa kamati hiyo baada ya uchaguzi uliofanyika jana ambapo jumla ya wajumbe kumi wamepatikana.
Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa, Mhe. Juma Khatibu(katikati) akizungumza wa kikao cha kwanza cha Kamati ya Uongozi ambapo wajumbe wake wamechaguli wa jana tarehe 27 Agoisti 2021. Kutoka kushoto ni Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa, Mohammed Ally Ahmed na Makamu Mwenyekiti wa Baraza hilo ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu CCM Bara, Bibi. Christine Mndeme.

Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia hotuba ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi(hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa Kamati Mpya ya Uongozi wa Baraza la Vyama vya Siasa leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa jijini Dar es Salaam. (Picha na: ORPP)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad